Thursday, January 14, 2016

WAZIRI MBARAWA AJISAJILI MFUMO WA MAHUDHURIO WA KIELEKTRONIKI.

W1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kulia), akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya mawasiliano ni Profesa Faustin Kamuzora
W2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akijisajili katika mfumo wa mahudhurio wa elektoniki (kulia), ni Afisa Utumishi Bi, Elizabeth Maduhu akimwelekeza.
W3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akifungua mlango kwa kutumia mfumo wa mahudhurio wa elektroniki baada ya kujisajili.
W4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akisaini kitabu cha mahudhurio baada ya kujisajili katika mfumo wa mahudhurio wa elektroniki katika ofisi za sekta mawasiliano.
W5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa wa (kwanza kulia), akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora (katikati) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Dakta Maria Sasabo.
………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Prof. Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa taasisi zote za Serikali kuwa na mfumo wa mahudhurio kwa njia ya kielekroniki electronic attendance registration (EAR).
Akizungumza mara baada ya kujisajili katika ofisi za sekta ya mawasiliano Prof. Mbarawa amesema kwa kuanzia utaratibu huo utaendelezwa katika sekta Uchukuzi na Ujenzi na kisha utafungwa katika taasisi zote za Serikali ili kuhakikisha watumishi wa umma wanafika ofisini kwa wakati na kupunguza utoro.
“Hakikisheni watumishi wote wanatumia mfumo huu wa kielektroniki ili kudhibiti utoro na kuwezesha wafanyakazi kufanyakazi kwa muda unaokubalika kiserikali ”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Mbarawa amewataka wafanyakazi wa mapokezi kuacha kuwafungulia wafanyakazi watoro na wanaochelewa kazini kuingia ofisini ili kuwezesha mfumo kutambua watumishi watoro na hivyo kuchukuliwa hatua stahiki.
Amesisitiza kuwa mfumo huo utakapofungwa katika taasisi zote za umma utadhibiti watoro kwa kuwa unaweka kumbukumbu ya muda mtu anaokuwa kazini na hivyo kuwawezesha viongozi kupata taarifa sahihi za mahudhurio.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...