Wednesday, January 13, 2016

RAIS MSTAAFU, DK ALI HASSANI MWINYI ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA SAYANSI YA JAMII YA CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA AFRIKA (IUA)

  Rais Mstaafu wa Tanzania, MzeeAli Hassani Mwinyi (katikati) akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) na Rais wa Sudani ambaye pia ni mkuu wa chuo hicho, Omar al-Bashir (wa pili kulia) mjini Khartoum, Sudani  hivi karibuni.
 Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (wa pili kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa zamani wa Mahakama Kuu ya Saudia, Abdulrahman Alsheikh Al Ashum alipotembelea Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) mjini Khartoum hivi karibuni na kutunukiwa Shahada ya Heshima (PHD) ya Sayansi ya Jamii ya chuo hicho na Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Sudani, Omar al-Bashir. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya   Munazzmat Al-Dawa wa Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Khalid A. Abdullah na kulia ni mke wa Mzee Mwinyi, Mama Khadija Mwinyi.
 Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (katikati) akisalimiana na baadhi ya watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) mjini Khartoum, Sudani  hivi karibuni ambapo pia alitunukiwa Shahada ya Heshima (PHD) ya Udaktari wa Sayansi ya Jamii ya chuo hicho na Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Sudani, Omar al-Bashir (hayupo pichani).
Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (wa pili kulia) akipokea nishati kutoka kwa Katibu Mkuu wa Taasisi ya  Munazzmat Al-Dawa, Abdulrahim Ali Ibrahim kutokana na mchango wa mzee Mwinyi katika kusaidia mipango na shughuli za taasisi hiyo barani Afrika hususani nchini Tanzania.  Rais mstaafu alitembelea nchini Sudani hivi karibuni ambapo akiwa huko alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (PHD) ya Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA). Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya   Munazzmat Al-Dawa wa Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Khalid A. Abdullah, Sheikh Athumani Kaburu wa Tanzania na waalikwa wengine. (Picha na Peter Mgongo)

 Rais Mstaafuwa Tanzania, Ali Hassani Mwinyi (katikati) akilakiwa na wenyeji wake baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Khartoum nchini Sudani hivi karibuni ambako pamoja na mambo mengine alitunukiwa shahada ya udaktari wa heshima ya sayansi ya jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) kutokana na mchango wake katika kusaidia maendeleo ya elimu nchini Tanzania na Afrika.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...