Sehemu ya waandishi wa habari wakishuhudia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akisaini hati ya makubaliano na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen na Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha wakishuhudia.Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen (kulia) akisaini hati ya makubaliano na Benki ya NMB itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha, tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB kwa kushirikiana na Kampuni maarufu kwa uuzaji wa matrekta ya John Deere zimeingia makubaliano ili kufanikisha kuwakopesha matrekta wakulia wanaochipuki kwa lengo la kuwawezesha waendelee kufanya vizuri kwenye kilimo cha kisasa.
Katika makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Banki ya NMB imekubali kutoa mkopo ambao utamuwezesha mkulima kununua trekta hilo huku akiurejesha taratibu, Hata hivyo Kampuni ya John Deere itatoa mafunzo ya kilimo cha biashara kwa mkulima aliyenufaika na mkopo huo pamoja na kumfundisha matumizi bora ya kifaa hicho cha kilimo.
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi alisema benki yao inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo na inavyochangia kukuza uchumi wa Tanzania hivyo kuamua kuwawezesha wakulima ili kuchochea ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
"...Upatikanaji wa mikopo kwa wakulima siku za nyuma ulikuwa ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya kilimo...hivyo makubaliano haya yanakuja kuleta suluhisho kwa wakulima hasa katika eneo la kupata vifaa muhimu vya kilimo cha kisasa kama matrekta yanayoendana na mabadiliko ya teknolojia," alisema Mponzi.
Alisema kwa kutambua mchango wa sekta ya kilimo tayari Benki ya NMB imewasaidia wakulima wadogo zaini ya 600,000 kupata mitaji ya mikopo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao anuai ya kilimo pamoja na kuendesha mafunzo ya kijasiliamali kuwajengea uwezo makundi yote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen alisema mikopo hiyo inayotolewa kwa wakulima inalengo la kuwainua wakulima wadogo ili waweze kubadili kilimo chao kuwa kilimo endelevu kinachotumia vifaa vya kisasa yakiwemo matrekta ya kilimo, kuvunia na kusafirisha mazao kutoka shambani hadi eneo linalokusudiwa.
"Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wadogo katika nchi za Afrika, John Deere kwa kushirikiana na NMB tunategemea kuweka mifumo itakayowawezesha wakulima wadogo ili kuleta ufanisi katika shughuli nzima ya kilimo. Ufanisi katika manunuzi ya pembejeo, uzalishaji na pia matumizi ya teknolojia za kisasa (mbegu, mbolea na hata vitendea kazi-mashine) na hata ufanisi katika kutafuta masoko ya mazao yao mojakwa moja," alisema Westhuizen.
No comments:
Post a Comment