Mwanamitindo wa Tanzania ambaye anafanya kazi za mitindo nchini Marekani, Flaviana Matata amezindua bidhaa za urembo za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY, amezindua bidhaa hiyo mbele ya waandishi wa habari na kuomba wanawake na watumiaji rangi za kucha wamuunge mkono kwani ni bidhaa ambayo ipo kwenye soko kwa kipindi hiki kwani kila mwanamke anapenda kupendeza. Kulia ni Afisa mtendaji mkuu wa Shear Illution Ltd, Shekha Nasser akiwa ni mmoja wa wasambazaji wa kipodozi cha Kucha ambazo zimezinduliwa leo.
Wakati huhuo amewapongeza wote waliochangia katika kufanikisha yey kujulikana kimataifa.
Afisa mtendaji mkuu wa Shear Illution Ltd, Shekha Nasser akizungumza na waandishi waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kushirika katika uuzaji wa vipodozi vya kucha ambavyo vitakuwa kikiuzwa katika duka lake.
Bidhaa za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY amazo zimezinduliwa na mwanamitindo Flaviana Matata jijini Dar es Salaam leo.
Bidhaa hizo zitakuwa zikipatikana kwenye maduka mbalimbali na Saluni za Pikasso, Shear Illution Ltd na Zuri Cosmestics zilizopo jijini Dar es Salam kwa shilingi elfu tano tuu.
No comments:
Post a Comment