Thursday, January 14, 2016

CLOUDS TV YAINGIA RASMI KWENYE KING’AMUZI CHA DSTV “CHANELI 294”

MultiChoice Africa inapenda kuwatangazia wateja wake na watanzania kwa ujumla  kuwa  Clouds TV sasa imeingia rasmi kwenye DStv.

Kile kilio cha muda mrefu cha watazamaji na wapenzi wa Clouds TV juu ya Clouds TV kukosekana kwenye king'amuzi cha DSTV kimesikika na sasa Clouds TV imeingia rasmi ndani ya DStv.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja  Uendeshaji  MultiChoice Tanzania, Ndugu Ronald Baraka Shelukindo,  amesema baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya Clouds TV na Multichoice Africa  kuhusu Clouds TV kuingia katika king'amuzi cha DStv, MultiChoice Africa na Clouds TV wamefikia muafaka ambapo watazamaji na wapenzi wa Clouds TV  wenye ving'amuzi vya DStv watapata uhondo wa Clouds TV ndani ya DStv.

Akiongezea, Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania , Ndugu Salum Salum  ameelezea furaha ya kampuni yao na akasema,  wakati mwingine walikuwa wanashindwa kufikia lengo la kupata wateja wengi zaidi kutokana na kukosekana kwa  Clouds TV  “hivyo kuanzia sasa, tuna imani kuwa idadi ya wateja itaongezeka maradufu!”.

Clouds TV itaanza kupatikana rasmi ndani ya DStv tarehe 14 Januari 2015, kwenye Chaneli 294, katika  vifurushi  vyake vyote ikiwemo; Premium, Compact Plus, Compact , Family na kifurushi cha DStv Bomba.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...