Wednesday, January 27, 2016

KONGAMANO LA KUJADILI MPANGO WA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU (ESDP) KWA MWAKA 2017 – 2021 LAFANYIKA DAR ES SALAAM

1
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salumu Mnjagila (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa  kongamano la siku mbili  la kujadili vipaumbele kwa miaka mitano ijayo vinavyotakiwa katika kuandaa mpango ili kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua na ubora zaidi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, Teknolojia na Utamaduni (UNESCO) limepanga kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara (katika), Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues.kongamano hilo limewakutanisha wadau wa elimu pamoja na mashirika ya dini.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG)
2
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi.Zulmira Rodrigues akifafanua kuhusiana na kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuifanya kuwa bora na iliyo na usawa kwa makundi yote ya jamii kwa matokeo mazuri ya baadae.
3
56
Wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi pamoja na wadau wa elimu wakifuatilia mada wakati wa kongamano la siku mbili  la kujadili vipaumbele vinavyotakiwa katika kuandaa mpango ili kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua na ubora zaidi,
????????????????????????????????????
Baadhi ya watumishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia (UNESCO) wakifurahia jambo wakati wa kongamano la siku mbili  la kujadili vipaumbele vinavyotakiwa katika kuandaa mpango ili kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua na ubora zaidi,

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...