Basi la Kampuni ya BM linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam - Morogoro, limepata ajali usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mikese Mkoani Morogoro, na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 43 kujeruhiwa. Basi hilo liligongana na gari lingine na kutumbukia kwenye Korongo.
Chanzo cha ajali hiyo, inadaiwa ni mwendo kasi wa Basi hilo uliopelekea kushindwa kusimama baada ya kukuta Lori lililokuwa limeharibika na kuegeshwa pembeni, huku upande mwingine kukiwa na Lori lingine likipita.
Basi la Kampuni ya BM linavyoonekana baada ya kupata ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment