Monday, August 10, 2015

KITUO CHA RADIO 5 CHASHINDA NAFASI YA KWANZA MAONYESHO YA NANENANE ARUSHA

SAM_4950
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akiwa anamkabidhi kikombe Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya mara baada yakituo cha Radio5 kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha.
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4952
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa ameshikilia kikombe walichoshinda katika maonyesho ya nanenane
SAM_4977
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya akiwa na timu yake ya ushindi mara baada ya kituo hicho kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha
SAM_4970
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa anamkabidhi funguo ya pikipiki kwa Mkuu wa wilaya Monduli Jowika Kasunga zawadi ya mshindi wa kwanza katika kilimo
SAM_4974
Wafanyakazi wa Radio 5 katika nyuso za furaha
……………………………………
Kituo cha Radio 5 kilichopo jijini Arusha kimeshika nafasi ya kwanza katika maonyesho ya nanenane kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kikombe na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya alisema kuwa wanafuraha kubwa kwa kupata ushindi huo
Alisema kuwa Radio 5 imekuwa ikiwapa kipaumbele wakulima ambapo wamekuwa wakiandaa vipindi vya kilimo ambapo katika studio zao huwaalika wataalamu mbalimbali wa kilimo lengo ni kuwapa elimu kuhusu kilimo cha kisasa
Pia Radio hiyo imekuwa ikiwapatia wakulima msaada wa mbegu,mbole na wamekuwa wakiwatembelea mara kwa mara kujua maendeleo yao katika masuala ya kilimo
“Vipindi vyetu vya kilimo vimekuwa vikitupa tuzo mbalimbali nah ii leo katika maonyesho haya pia tumepata tuzo”alisema Keiya
Aidha alisema kuwa wamekuwa wakitoa zawadi kila mwaka kwa mkulima bora atakayechaguliwa na TASO ambapo wametoa pikipiki aina ya powew king yenye thamani ya shilingi milioni mbili,mbole pamoja na mbegu
Hata hivyo alitoa shukrani zake kwa mkurugenzi wa kituo hicho Bw,Robert Francis kwa kuwawezesha wafanyakazi kufanya vizuri katika maonyesho hayo huku akisema kuwa anatimu nzuri inayojituma na yenye uwezo mkubwa kikazi
Aliwashukuru wadhamini SBs(pepsi),Kishen enterprises limited,Upendo kwa mama foundation,Grandmaster records,Atown records na wote waliojitokeza kushirikiana nao

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...