Monday, August 10, 2015

KIJANA MFUGAJI AWEZESHWA NA AIRTEL FURSA

  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikata utepe kuashiria kumkabidhi kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel. 
1) Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akifafanua jambo kwa kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), kabla ya kumkabidhi msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo (kushoto) na maafisa wa Airtel wa Mikoa ya Arusha na Manyara.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimpongeza Jonathan Tarimo (wa pili kulia), baada ya kumkabidhi msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo, Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel na Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara, Peter Kimaro.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa tatu kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. 

AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Airtel
Fursa “Tunakuwezesha” imemkabidhi kijana Jonathan Clement mkazi    Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha ng’ombe wawili, banda la kisasa pamoja na mafunzo ya biashara   ambayo itamsaidia kuinua biashara yake ya ufugaji na kumuongezea kipato chake.
Jonathan kijana mwenye umri wa miaka 21 na elimu ya kidato cha nne  amekabidhiwa mtaji huo ambapo awali alikuwa na ngomb’e wawili na banda  lililochoka  na  alikuwa na changamoto ya elimu ya ufugaji na madawa ya mifugo.
Jonathan ameishukuru kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kumpatia msaada huo amesema  “biashara yangu ya ufugaji sasa itapiga hatua. Naamini miaka michache ijayo nitakuwa na mifugo mingi sana na soko langu la maziwa litakuwa kwa kasi. Na vile vile itaniwezesha kuinua familia na biashara yangu kwa ujumla”.

“Hii ni bahati ya peke kwangu kutoka Airtel, kwani ni vijana wengi sana wanatamani kupata hivi nilivyovipata lakini hawakupata bahati hii. Nawahimiza vijana wengine wasikate tamaa na  wajitokeze kwa wingi kwani Airtel Fursa ipo kutuwezesha vijana”.

Akizungumza baada ya makabidhiano, Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, alisema “mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na kuwakwamua kiuchumi. Jonathan amepitia changamoto nyingi kufikia hapa alipo alianza na ngombe wa kukopeshwa kutoka kwa mjomba wake kwa makubaliano kwamba atakapopata ndama wa kwanza atakuwa wa kwake. Lakini leo hii tumemuwezesha kuwa na jumla ya ng’ombe watatu kwenye zizi lake”.
“Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” imempatia msaada huu Jonathan baada yakuridhishwa na hatua ya ufugaji pamoja na kuonyesha nia yakuwa mfugaji bora hapa nchini” alisema.

Bayumi aliwataka vijana wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huu unawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao..
“Program hii inahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini alisema.
Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma
ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com<mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com

No comments:

RAIS SAMIA APONGEZWA KUWEZESHA UJENZI OFISI KUU WMA

  ✅ Katibu Mkuu Viwanda na Biashara amshukuru Rais kutumia vyema fedha za Watanzania ✅Akagua ujenzi Jengo la WMA na kukiri kuridhishwa ✅Mten...