Friday, June 12, 2015

WATOA HUDUMA MKOANI LINDI WAASWA KUCHANGAMKIA MIKOPO INAYOTOLEWA NA NHIF ILI KUBORESHA HUDUMA ZA MATIBABU-RAS LINDI

3
Meneja wa Mfuko Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akifafanua dhamira ya mfuko katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya afya, kupitia mikopo iliyoboreshwa ,kwani hadi kufikia mwezi Mei. 2015 watoa huduma wa mkoa wa Lindi wameweza kukopa takribani 135mil. ambapo kati ya fedha hizo hospitali ya mkoa ilikopa ultra sound yenye thamani ya 54Mil. Amesisitiza kuwa huduma zinapoimarika  hususani upatikanaji wa dawa wananchi hawatasisita kuchangia kwenye CHF.
Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Lindi Grayson Mwaigombe amewataka  waganga wakuu wa hospitali kuanzia ya mkoa na wilaya,kuchangamkia mikopo ya riba nafuu inayotolewa na NHIF, ili waweze kuboresha huduma na pia kuwa chanzo kingine cha mapato ya hospitali,kwani wananchi kwa sasa wanahitaji huduma bora na stahiki, aliyesema hayo wakati wa elimu ya uhamasishaji watoa huduma wa Serikali, mashirika ya dini na watu binafsi waliosajiliwa na mfuko,kuchangamkia fursa ya mikopo ya vifaa tiba, ukarabati wa maeneo ya kutolea huduma , dawa na vitendanishi,Mkoani Lindi jana kwenye ukumbi wa mikutano wa hospitali ya sokoine.
2
Washiriki wa mafunzo hayo ambayo yaliwajumuisha viongozi wa halmashauri Lindi na waganga wakuu na wenyeviti wa halmashauri, watoa huduma wa binafisi wakimsikiliza mgeni rasmi kaimu katibu tawala hayupo pichani.
4
Mtoa elimu afisa kutoka makao makuu ya mfuko isaya shekifu akiwasilisha mada inayotoa miongozo na taratibu za maombi ya mikopo,ambapo aliwataka watoa maamuzi kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za matibabu kwani kutachochea wananchi wengi kujiunga na CHF, hivyo kuongeza mapato ya hospitali, kwa sasa mfuko umetenga jumla ya 2bilioni ili watoa huduma wa serikali,binafsi na mashirika ya dini waweze kukopa. 
5
Mganga mfawidhi kituo cha afya mjini kati Lindi Dr. Zulfa Msami akiuliza jambo baada ya uwasilishwaji wa mada

No comments:

RAIS SAMIA AWAINUA PIKIKIPI 37 MAAFISA UGANI WA KILIMO KIBAHA TC

  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA Halmashauri ya Kibaha mji imepokea jumla ya pikipiki zipatazo 37 kutoka serikalini kupitia Wizara ya kilimo ...