Friday, June 12, 2015

WASIRA AWAIMIZA WAKAZI WA MTWARA KUWEKEZA KATIKA UZALISHAJI WA MAZAO YA KILIMO NA UVUVI

 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira akiongea na baadhi
ya wanachama wa CCM mkoani Mtwara alipofika kuomba kudhaminiwa
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira akipokewa na baadhi
ya wanachama wa CCM mkoani Mtwara alipofika kuomba kudhaminiwa
…………………………………………
Na Woinde Shizza
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira,amewahimiza
wakazi wa Mtwara kuwekeza katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na uvuvi ikiwa
ni sehemu ya shughuli za kiuchumi zitakazowanufaisha kutokana na kugundulika
kwa gesi asilia katika ukanda wa kusini mwa nchi.
 
Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda alikuwa akizungumza
na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliomdhamini ili apitishwe na chama
hicho kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Alisema ingawa zipo fursa nyingi zitakazowanufaika
Watanzania  kutokana na sekta hiyo mpya
(gesi), lakini mazao ya kilimo na uvuvi yanaweza kuwa miongoni mwa shughuli
zitakazowanufaisha wananchi wengi hasa wa hali ya chini.
Mtwara ni eneo lililowahi kukumbwa na machafuko kutokana
na hisia tofauti zilizokuwapo kuhusu manufaa yanayopaswa kuwafikia wakazi wa
mkoani Mtwara, hasa kuhusu ujenzi wa viwanda na kuibadili gesi ili
itakaposafirishwa isiwe katika mali ghafi.
Hata hivyo, Wasira alisema anatarajia kufungua fursa
nyingi zaidi za kiuchumi kwa ajili ya wananchi kama atateuliwa na CCM na
hatimaye kushinda katika Uchaguzi huo
Hakuelezea kwa undani kutokana na kuwa wakati wa kampeni
bado haujafika, bali sasa hivi anatafuta udhamini ndani ya CCM.
Wakati huo, Wasira na mtia mwingine, Makongoro Nyerere,
wameelezea kuridhika na namna wanavyoshiriki mchakato wa kusaka Urais kwa
kutumia magari, tofauti na watia nia waliowekeza fedha nyingi kiasi cha kutumia
usafiri wa angani katika maeneo mengi.
Waliyasema hayo walipokutana kwenye ofisi za CCM mkoa wa
Mtwara, ambapo Makongoro, alirukaruka na kumkumbatia Wasira. Tukio hilo lilitafsiriwa
kuwa ni ishara za umuhimu wa kufanya ushawishi kwa amani pasipo kuiathiri CCM,
wanachama ama Watanzania kwa ujuma.
“Hizi ndizo siasa tunazozitaka ndani ya CCM na Tanzania
yetyu, sio wagombea wengine wanaotumia utajiri na fedha zao kuwakandamiza
wadogo na kuibua mafarakano kwenye jamii,” akasikika kiongozi mmoja wa CCM
(jina tunalo) akisema.
Wasira, alikwenda pia katika mkoa wa Lindi ambapo
alifadhiliwa. jana (alhamis) ataelekea mkoani Mwanza kuendelea na ziara ya
kuomba udhamini kwa wana-CCM wa mikoa ya kanda ya Ziwa Victoria.

No comments:

RAIS SAMIA AWAINUA PIKIKIPI 37 MAAFISA UGANI WA KILIMO KIBAHA TC

  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA Halmashauri ya Kibaha mji imepokea jumla ya pikipiki zipatazo 37 kutoka serikalini kupitia Wizara ya kilimo ...