Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamyange akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri wa
Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC) na semina ya wadau wa usafiri wa anga Dar es Salaam jana.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamyange akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa
Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC, Shaban Mtambalike wakati wa uzinduzi wa baraza hilo la nne tangu kuanzishwa kwake.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri wa
Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), Hamza Johari akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi huo.

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamnyange (walioketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza hilo na wadau wa Sekta ya usafiri wa Anga.
****************
Na Father Kidevu Blog
USHINDANI mdogo katika utoaji wa huduma za usafiri
wa anga kutokana na kuwepo kwa mashirika machache ya ndege yanayotoa huduma
nchini.

Hayo yalibainishwa Dar es Salaam juzi na Katibu Mtendaji wa baraza la Ushauri wa
Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), Hamza Johari wakati
wa uzinduzi wa baraza hilo na semina kwa wadau wa usafiri wa anga nchini.

Johari alisema endapo kama nchini kungekuwa na
watoa huduma wengi wa usafiri wa anga basi kungepelekea kushuka kwa gharama za
usafiri na kuwepo kwa huduma bora miongoni mwao.

“Siku zote tunaamiani kama ushindani wa kutosha
gharama zinakwenda chini, huduma zinakuwa bora, na ni mdogo kwasababu soko na
miundominu haijaweza kutandaa nchi nzima, ”alisema Johari.

Aidha Johari alisema pindi nchi itakapokuwa na
miundombinu bora ya viwanja vya ndege, na utaratibu mzuri wa huduma za anga
nchini anaamini huduma zitaboreka zaidi.

Mapema akifungua baraza hilo, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange amewataka kuwa karibu na wadau wa sekta
ya usafiri wa anga nchini ili kuweza kutoa huduma bora na zenye ufanisi nchini.

Mwamunyange alisemwa ipo haja ya baraza kulifanyia
kazi dhana ya ushirikishwaji na utoaji wa elimu kwa walaji kuwa ya vitendo
zaidi.

“ Baraza linatakiwa kuwashirikisha wadau wake
katika mambo mbalimbali yanayoendelea katika seklta nzima ya usafiri wa anga
lakini pia wanapaswa kutoa elimu ya mara kwa mara ya haki na wajibu wa
mlaji,”alisema Mwamunyange.

Baraza lina takiwa kuangalia maslahi ya mtumiaji
wa huduma za usafiri wa anga na kutoa elimu ambayo itamfanya mlaji awe na
uwelewa wa kutosha wa huduma za anga.

Aidha Mwamunyange amesema kwa sasa huduma za
usafiri wa anga nchini zinakabiliwa na changamoto kutoka kwa walaji ambapo
wanashindwa kutofautisha huduma zitolewazo na mashirika yatuayo huduma za
gharama nafuu nay ale yaliyozoeleka.

Wadau wa usafiri wa anga pia walipata fursa ya
kushiriki semina baada ya uzinduzi huo na mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni
pamoja na huduma kwa wateja, uwajibikaji wa mtoa huduma anaposababisha madhara,
ndege za bei nafuu na masuala ya usalama.

Uzinduzi wa baraza hilo la nne la Ushauri wa
Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC), baada ya kuteuliwa
na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ambapo pia wajumbe wa Baraza lililopita
waliagwa.

No comments:
Post a Comment