Tuesday, June 02, 2015

TAASISI YA UTT-PID CHINI YA WIZARA YA FEDHA YAPANUA BARABARA ENEO LA MRADI WA VIWANJA LINDI


 Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi.
Baada ya kupima na kufanikiwa kuuza viwanja zaidi ya 2,500 katika fukwe za Mabano na Mmongo kwa ushirikiano na Manispaa ya Lindi, Mradi huo umeingia katika hatua ya upanuzi wa barabara kuu na za mitaa ndani ya mradi ambapo kwa ushirikiano huo zaidi ya Shilingi Billion 1 zinatarajiwa kutumika mpaka kukamilika kwake.
Mradi huo mkubwa zaidi nchini katika upimaji wa viwanja Manispaa ya Lindi ulifadhiliwa na Taasisi ya UTT-PID utekelezaji wake ulianza mapema mwaka 2013 na sasa uaandaji wa hati kwa wanunuzi upo katika hatua ya mwisho baada ya kila mteja wa kiwanja kufanikiwa kuweka saini kwa hati zao katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi kwenyewe.
 Uchongaji wa hatua za awali wa Barabara ukiendelea katika eneo la Mradi. Ujenzi wa barabara hizi unatarajia kukamilika kabla ya wanunuzi kuuanza ujenzi wa makazi yao katika eneo la mradi.
Uwekezaji huo ukiendelea pia Taasisi hiyo kwa ushirikiano huo na Halmashauri ya Lindi inatarajia kuingia katika awamu ya pili ya Mradi wa upimaji viwanja katika fukwe hizo ambapo zaidi ya viwanja elfu tano vitapimwa na kuuza kwa wananchi wote. Utekelezaji wa awamu ya pili bado upo kwenye hatua za awali na unatarajia kuuanza ndani ya mwaka huu 2015.
 Viwanja vya Mabano na Mmongo vipo katika fukwe nzuri na vikipata upepo mwanana kutoka bahari ya Hindi.
Toka kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000 vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. Pia Taasisi imewekeza katika miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.
 Upanuzi huu wa barabara utafanyika mpaka kwenye fukwe kuwapa nafasi wakazi wa eneo husika kutembelea maeneo ya fukwe hizo
Zaidi ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog).

No comments:

Rais wa Sierra Leone Awasili nchini

Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wak...