JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TANZIA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mhe. EUGEN ELISHIRINGA MWAIPOSA kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 June 2015 nyumbani kwake Dodoma ambako amekuwepo kushiriki Mkutano wa Bunge la Bajeti.
Mwili wa Marehemu utaagwa kesho tarehe 3 Juni 2015 kuanzia saa 4 asubuhi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na baadaye mwili kupelekwa nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam.
BWANA alitoa, BWANA ametwaa. Jina la BWANA lihimidiwe. Amina!
Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dodoma,
2 Juni 2015.
No comments:
Post a Comment