Monday, June 23, 2025

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ATEMBELEA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA VIFAA TIBA NCHINI ITALIA










ROMA, ITALIA – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, ametembelea kampuni ya kimataifa ya uzalishaji wa vifaa tiba, Health 3000, iliyopo mjini Roma, Italia, leo tarehe 23 Juni 2025.

Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni hiyo, akiwemo Mwenyekiti Maurizio Flammini na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Eleonora Flammini. Mazungumzo hayo yamejikita katika kujadili fursa za ushirikiano kati ya Tanzania na kampuni ya Health 3000, hasa katika sekta ya huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya matibabu kwa njia ya mtandao (Telemedicine).

Health 3000 ni miongoni mwa kampuni zinazofanya kazi chini ya mwamvuli wa FG Group, ambayo imejikita katika maendeleo ya huduma za afya kupitia uzalishaji wa vifaa tiba vya kisasa.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango yupo nchini Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ubia wa Maendeleo kati ya Afrika na Serikali ya Italia, maarufu kama Mattei Plan, pamoja na kushiriki mikutano mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili.

Ziara hii inaendelea kudhihirisha dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuimarisha mahusiano ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi.

No comments:

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ATEMBELEA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA VIFAA TIBA NCHINI ITALIA

ROMA, ITALIA – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, ametembelea kampuni ya kimataifa ya uzalis...