Monday, December 01, 2014

BALOZI MDOGO WA TANZANIA DUBAI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MDOGO WA SAUDI ARABIA DUBAI


 Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga amekutana na Balozi Mdogo wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu wa Mabalozi wadogo nchini humo (Dean of Diplomatic Corps)  Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia.  Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga akiagana na Balozi Mdogo wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu wa Mabalozi wadogo nchini humo (Dean of Diplomatic Corps)  Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia.
Mhe. Mjenga alienda kumtembelea ili kuomba ushiriki wake pamoja na Mabalozi Wadogo wote kwenye kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii nchini Tanzania, litakalofanyika tarehe 17 Disemba 2014.
Mhe. Emad Madani amesema atashiriki vikamlifu kwenye kongamano hilo huku akisema kuwa Tanzania na Saudi Arabia ni nchi rafiki wa siku nyingi, na hivyo basi wapo tayari kuomba taasisi ya utalii ya Saudi Arabia kushiriki pia.
Aliahidi kuwaomba Mabalozi Wadogo wote washiriki. Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...