Wednesday, October 01, 2014

Wanasiasa Wakongwe wa Kenya Wamtembelea Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli - CCM Edward Lowassa Monduli


Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa(kulia)akiwakaribisha mawaziri wa zamani wa Kenya  William ole Ntimama(tai nyekundu) na John Keen(kushoto) nyumbani kwake Monduli. Wanasiasa hao wakongwe na wenye ushawishi mkubwa katika eneo la Maasai Land nchini Kenya walimtembelea Mh Lowassa ambaye ni Laigwanan mkuu wa wamasai wote Afrika mashariki, na kujadiliana naye masuala mbalimbali lakini zaidi ni juu ya suala la ardhi ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa jamii ya wamasai.

Wazee hao wanatarajiwa kuudhuria semina maalum katika jimbo la Monduli wiki ijayo kuzungumzia tatizo la ardhi.Semina iliyoandaliwa na Mh Lowassa itawashirikisha viongozi wote wa wilaya hiyo pamoja na wakuu wa kimila.Akizungumzia suala la ardhi mzee John Keen alisema mtu anayeuza ardhi anauza utajiri na kununua umasikini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...