Monday, August 04, 2014

MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA ATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA MKOANI LINDI

1Afisa Mshiriki wa Maonesho ya Wakulima na Wafugaji katika Banda la Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda(kushoto) akitoa maelezo ya kitalaam kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Regina Chonjo(kulia) namna viatu vya Ngozi vinavyotengenezwa na Jeshi hilo katika Kiwanda chake cha Gereza Karanga, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyoshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo ya Kitaifa Mkoani Lindi.
2Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Regina Chonjo(wa pili kushoto) akiangalia Mbegu ya Ufuta inayozalishwa na Jeshi la Magereza kupitia miradi mbalimbali ya Kilimo katika Magereza ya Kilimo hapa Nchini(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Tusekile Mwaisabila.
3Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Regina Chonjo akikagua Bustani ya Shamba Darasa iliyopo katika Banda la Jeshi la Magereza katika Viwanja vya Maonesho vya Ngongo, Mkoani Lindi. Bustani hiyo iliyostawishwa kwa kufuata Kanuni za Kilimo Bora na Biashara inatumika kutoa elimu kwa Wakulima wanapotembelea Banda hilo katika Maonesho haya ya Kimataifa.
5Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza ili kujionea shughuli mbalimbali za Kilimo na Ufugaji zinazofanywa na Jeshi hilo katika Maonesho hayo ya Nane Nane.
8Lango Kuu la kuingia katika Banda la Jeshi la Magereza katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Ngongo, Mkoani Lindi. Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyoshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...