Wednesday, August 27, 2014

UMOJA WA MACHIFU TANZANIA (UMT) WAWASILISHA MAPENDEKEZO YAO KUHUSIANA NA RASIMU YA KATIBA MPYA.

PIX 1Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu akiwaeleza jambo Wawakilishi wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) kuhusu mapendekezo yao waliyoyawasilisha kwake kwaajili ya Katiba Mpya jana 26 Agosti, 2014.
PIX 2Chifu John Nyanza (aliyekaa katikati) wa kutoka Magu akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya alipokutana naye jana 26 Agosti, 2014. kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
PIX 3.Chifu Agnes Ndaturu (kushoto) wa kutoka Ntuzu, Bariadi akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya alipokutana naye jana 26 Agosti, 2014. kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
PIX 4.Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) akipokea mapendekezo ya maoni toka kwa Chifu John Nyanza alieuwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) jana 26 Agosti, 2014.kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
PIX 5.Baadhi ya Waandishi wa Habari walikifuatilia uwasilishwaji wa mapendekezo toka kwa Machifu waliouwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) jana 26 Agosti, 2014.kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
26/08/2014.
UMOJA wa Machifu wa Tanzania (UMT) kupitia wawakilishi wake, jana 26 Agosti, 2014 umewasilisha nyongeza ya mapendekezo yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akiuwakilisha Umoja wa Machifu Tanzani (UMT), Chifu kutoka Magu John Nyanza amemueleza Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kuwa wanaishauri Serikali kutayarisha mkakati wa Kitaifa wa Utamaduni kwa kuwashirikisha wadau wakuu wa masuala ya Utamaduni ili mpango mkakati huo uwe na Dira ya Utamaduni itakayobainisha cha kufanya ili kujenga, kuhamasisha na kuendeleza Utamduni katika maeneo yote nchini.
“Chifu kutoka Magu, John Nyanza amesema kuwa lengo la kuwasilisha mapendekezo hayo kwaajili ya kusisitiza masuala mazuri ya Utamduni kuendelea ili kuweza kudumisha madili kwa nia nzuri ya kudumisha amni na ushirikiano”. Alisema Chifu Nyanza.
Naye Chifu kutoka Ntuzu, Bariadi Chifu Agnes Ndaturu ameeleza kuwa mapendekezo yao yatasaidia kuweza kuwatambua waganga wa Jadi ambapo hapo zamani , mganga wa Jadi alikuwa anatambulika na kufanya kazi katika eneo husika analotoka, lakini hivi sasa waganga wengi wa jadi wamekuwa na tabia ya kufanya kazi zao bila mipaka.
”Mapendekezo haya yatasaidia viongozi wa waganga wa jadi nchini kuwatambua wale waganga wanaokiuka maadili ya shughuli zao mfano mauaji ya Albino, kwakuwa kila kiongozi atakuwa anawatambua waganga wa eneo lake husika”. Alisema Chifu Ndaturu.
Aidha, Machifu hao wameongeza kuwa, Wajumbe wenzao waliowatuma kuwawakilisha wanasisitiza juu ya umuhimu wa Utamaduni kupewa nafasi rasmi katika Katiba mpya na Serikali ili pawepo na kipaumbele katika utekelezaji wake nchini.
Wakizungumza kwa kauli moja Umoja wa Machifu wa Tanzania wamesema kuwa suala la Utamaduni katika Rasimu ya Pili ya Katiba lifanyiwe marekebisho kwa kuzingatia mapendekezo yaliyoibainishwa huku msisitizo wao ukiwa katika Katiba kueleza wazi kuwa sera na Sheria mpya zitakazotungwa zihakikishe kuwa Tume ya Taifa ya Utamaduni inaanzishwa kisheria ili kusimamia masuala ya Utamaduni.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatotoa wasiwasi wawakilishi wa Umoja wa Machifu hao wa Tanzania aliokutana nao kwa kuwaeleza kuwa atayawasilisha katika Uongozi wa Kamati ya Bunge ambapo Kamati Ndogo ya Uongozi inatarajiwa kukutana leo jioni ili kuweza kuyajadili.
“Nimeyapokea mapendekezo yenu, kwakuwa Kamati zinaendelea na kazi ambapo wiki hii kamati zitakuwa zimemaliza kazi zake na hakutakuwa na nafasi tena ya kuyapokea mapendekezo na maoni mengine”. Alisema Samia.
Hivi karibuni, makundi mbalimbali yaliwasilisha mapendekezo yao ambapo baadhi ya makundi hayo yakiwemo Wafugaji, Wasanii na Wanahabari yaliwasilisha.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...