Friday, August 15, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI UTOAJI TUZO WA WANASAYANSI WACHANGA WA TANZANIA

01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa Wanasayansi wachanga kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Tanzania, iliyofanyika jana Agosti 13, 2014 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongero, John Andrea (wa pili kulia) na Thobias Clement, wakati wakimuelezea jinsi walivyoweza kufanya utafiti  na kugundua matumizi ya Kinyesi cha wanyama kuzalisha Umeme, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wanasayansi wachanga, yaliyofanyika jana Agosti 13, 2014 sambamba na utoaji tuzo za washindi wa maonesho hayo, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa Wanasayansi wachanga kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Tanzania, iliyofanyika jana Agosti 13, 2014 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (kulia) na Salma Khalfan (wa pili kulia) wakati wakimuelezea jinsi walivyoweza kufanya utafiti  wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wanasayansi wachanga, yaliyofanyika jana Agosti 13, 2014 sambamba na utoaji tuzo za washindi wa maonesho hayo, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakabidhi Tuzo washindi wa jumla wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (wa pili kushoto) na Salma Khalfan (wa tatu kulia) baada ya kutangazwa kuwa  washindi wa jumla katika maonesho ya Wanasayansi wachanga  kwa  kufanya utafiti  wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati  wa halfa ya utoaji Tuzo hizo wa wanasayansi wachanga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Agosti 13, 2014. Picha na OMR
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda ya maonesho.
04
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo baada ya kuwakabidhi Tuzo washindi wa jumla wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (wa pili kushoto) na Salma Khalfan (wa tatu kulia) baada ya kutangazwa kuwa  washindi wa jumla katika maonesho ya Wanasayansi wachanga  kwa  kufanya utafiti  wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati  wa halfa ya utoaji Tuzo hizo wa wanasayansi wachanga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Agosti 13, 2014. Picha na OMR
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi kushuhudia zoezi la utoaji tuzo za wanasayansi Wachanga lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana . Picha na OMR

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...