Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Jukwaa la Mabunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR) ukiongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye, Ikulu ndogo Tunguu, Zanzibar, tarehe 26 Oktoba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na ujumbe wa Jukwaa la Mabunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR) ukiongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye, Ikulu ndogo Tunguu, Zanzibar, tarehe 26 Oktoba, 2025. FP-ICGLR ni miongoni mwa misheni mbalimbali zilizowasili nchini kwa ajili ya uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Uganda, Dkt. Speciosa Wandira Kazibwe mara baada ya mazungumzo, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 26 Oktoba, 2025.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulioongozwa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Uganda, Dkt. Speciosa Wandira Kazibwe Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 26 Oktoba, 2025.
Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala ya demokrasia, amani na ushirikiano wa kikanda, huku ujumbe huo ukiwa miongoni mwa misheni mbalimbali ya kimataifa iliyowasili nchini kwa ajili ya uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.
Rais Dkt. Samia aliukaribisha ujumbe huo kwa ukarimu na kueleza kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, uwazi na kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora. Aidha, alisisitiza kuwa Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha hali ya usalama inabaki kuwa shwari katika kipindi chote cha uchaguzi.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Domitien Ndayizeye alitoa pongezi kwa Tanzania kwa maandalizi mazuri ya uchaguzi na kwa kuendeleza utamaduni wa kisiasa wa amani na umoja unaoitambulisha nchi hiyo katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Ameeleza kuwa FP-ICGLR, kama taasisi ya kikanda inayojikita katika kukuza demokrasia na utawala bora, itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha michakato ya kisiasa inatekelezwa kwa misingi ya haki, ushirikishwaji na utulivu.
Mazungumzo hayo yanaendelea kuonyesha dhamira ya Tanzania katika kushirikiana na jumuiya za kikanda na kimataifa katika kulinda amani, demokrasia na maendeleo endelevu barani Afrika.
#RaisSamia #FPICGLR #Uchaguzi2025 #TanzaniaInajengaDemokrasia #AmaniNaUmoja #Zanzibar












No comments:
Post a Comment