Majaji Bw. Venance Bahati (kushoto) na Bi. Costansia Gabusa (kulia) wakijadiliana jambo wakati wa kufanya tathmini ya mradi wa ukingo uliojengwa pembezoni mwa bahari kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko katika eneo la Mwarongo jijini Tanga. Ukingo huo umejengwa kwa msaada wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tongoni Bw. Mzihili Abeid (kushoto) akitoa maelezo mbele ya majaji waliotembelea maabara ya shule hiyo. Maabara hiyo imejengwa na kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia) akizungumza na jopo la majaji na sektretarieti kwenye maabara ya shule ya sekondari ya Tongoni iliyofadhiliwa na kampuni hiyo.
Jaji Venance Bahati (katikati) akiteta jambo na msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia). Kushoto ni Jaji Costansia Gabusa.
No comments:
Post a Comment