Saturday, August 02, 2014

ONESHO LA UCHEKESHAJI KUFANYIKA JUMAMOSI 2 AGOSTI 2014 JIJINI DAR ES SALAAM

1[2]
2[1]
Mchekeshaji ajulikanae kwa jina la kisanii wa Nchini Tanzania, Mc Pili Pili (kushoto), akiwa namchekeshaji kutoka nchini Kenya,Fred Omondi.
Mchekeshaji Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi.
‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.
Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.
‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.
Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band. 
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia.  ‘Usiku huo utakuwa ni maalumu kwa watanzania kufurahia Utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert. 
Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.
Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...