Monday, August 04, 2014

WANANCHI WA MKOA WA LINDI WAASWA KUJIUNGA NA CHF-ZAMBI

1 (8)Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Raphael Mwamoto  akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati alipotembea banda la Mfuko katika maonesho ya Nane Nane mkoani Lindi.
2 (7)Meneja wa Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akielezea namna Mfuko wa Afya ya Jamii unavyofanya kazi Mkoani humo.
3 (7)Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo ya huduma za Mfuko huo  ikiwa pamoja na kuupongeza kwa kazi nzuri.
4 (6)Ofisa Mdhibiti Ubora wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Timothy Mwasajone akitoa ushauri wa namna ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
5 (3)Sehemu ya wananchi wakisubiri kupata huduma katika banda la NHIF
Na Mwandishi Wetu, Lindi
SERIKALI imeutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendesha huduma za elimu ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza katika mikoa  yote hususani vijijini pamoja na upimaji wa afya bure ili wananchi watambue afya zao na hatimaye kuongeza uzalishaji katika sekta za kilimo na uvuvi na biashara kwa ujumla.
Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey Zambi wakati wa maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayoendelea mkoani Lindi ambapo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeshiriki na unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za elimu kwa Umma, usajili wa wanachama, upimaji afya bure ikiwemo saratani ya matiti.
Aidha alisisitiza kuwa mbali na huduma hizo nzuri zinazotolewa na Mfuko, ni vyema wananchi pia wakapata elimu juu ya umuhimu wa kujiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate matibabu bila ya usumbufu wowote.
“NHIF mnafanya kazi nzuri sana nawapongeza, na hata huduma mliyoileta huku Lindi katika kipindi hiki cha siku nane naamini wananchi wa maeneo haya watanufaika na huduma hizi hususan ya upimaji wa afya bure, hivyo ninachowaomba sasa ongezeni kasi hasa kwa kwenda vijijini ambako ndiko kuna kundi kubwa la wananchi,”
“Wakati mkifanya hizi huduma pia wahamasisheni wananchi kujiunga na Mifuko hii ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate huduma hata kama hawana fedha mfukoni,” alisema Naibu Waziri.
 Aidha alitoa mwito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi, Mtwara na wananchi wanaoishi jirani na mikoa hiyo kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii wakati wa maonesho haya kufika katika banda la NHIF ili kupata huduma ambazo zinatolewa bila malipo kwa wananchi lakini zimeghramiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Naye Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto, alisema kuwa NHIF kwa sasa inaendesha huduma hizi katika mikoa yote kwa lengo la kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa kujua  afya zao lakini pia umuhimu wa kupata huduma za matibabu kupitia Mifuko ya Afya ya Jamii.
Alisema kuwa kwa upande wa elimu juu ya faida za kujiunga na Mifuko ya Jamii, NHIF inao mpango wa elimu ya Kata kwa Kata ambayo inafanyika zaidi katika maeneo ya vijijini ili kuwahamasisha wananchi kujiunga na kunufaika na Mifuko hii.
“Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa sasa una ofisi zake kila Mkoa Tanzania ikiwemo Ofisi ya Zanzibar,  hivyo shughuli za elimu kwa umma na upimaji wa afya za wananchi hufanywa mara kwa mara na maofisa wa Mfuko walioko katika Ofisi zetu za  mikoani” alisema.
 Pia Ndugu Mwamoto aliendelea kusema kwamba matumizi sahihi ya fedha za tele kwa tele za CHF pamoja na fedha za matibabu zinazolipwa  na NHIF katika  vituo vinavyotoa huduma kwa wanufaika wa CHF na NHIF ni jambo muhimu sana. Alisema……..….’’ Fedha zinazolipwa na Mfuko pamoja na CHF ni fedha nyingi ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuboresha huduma za afya hasa upatikanaji wa dawa maeneo ya vijijini, kuna Halmashauri ambazo zimefanikiwa sana katika hili kwa mfano Nachingwea, Iramba, Igunga. Zingine ni Halamsahauri za Songea,Tanga ,Rombo,Singida na Mwanga. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaziomba Halmashaouri zingine  nchini kote ziige mfano huu’’,

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...