Friday, August 15, 2014

SHINDA NA LG KATIKA PROMOSHENI INAYOENDESHWA NA GARNET STAR LIMITED

IMG_5026
Mkurugenzi wa Garnet Star Limited Bw. Rajesh Darji akimkabidhi zawadi ya runinga yenye upana wa inch 55, aina ya Ultra HD Bw. Daniel V. Chuwa kutoka Moshi.
IMG_5035
Mkurugenzi wa Garnet Star Limited Bw. Rajesh Darji akimkabidhi mshindi zawadi ya runinga yenye upana wa inchi 32, Bw. Samwel Tungaraza kutoka Singida
IMG_5038
Mkurugenzi wa Garnet Star Limited Bw. Rajesh Darji akimkabidhi mshindi zawadi Bw. Abdulikadri Yusuph aliyeshimnda Mobile Photoprinter
IMG_5041
Mkurugenzi wa Garnet Star Limited Bw. Rajesh Darji akimkabidhi mshindi zawadi Dr. Eliausowy Meena aliyeshimnda Mobile Photoprinter
…………………………………………………………….
Garnet Star Limited, kwa kutambua umuhimu wa wateja wao inaendesha promosheni ambapo kwa kila mteja anayenunua kifaa cha picha na sauti kama vile TV Flat Screen, seti ya muziki, Hi-Fi na DVD ZA LG, chenye thamani ya kuanzia shillingi laki mbili na sabini na tano (275,000/=) anapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kama vile luninga ya inch 55 yenye uwezo wa picha ya HD, runinga ya inch 32, set ya muziki, na kichapisha picha ya mkono zote kutoka LG. Mwisho wa promosheni ilikuwa tarehe 31/July/2014 na Draw ilifanyika tarehe 4/8/2014. Na itatangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali, ambapo mshindi ataondoka na runinga ya LG yenye uwezo ya picha Ultra HD.
Promosheni hii ilifanyika katika maduka na supermarket mbalimbali yaliyothibitishwa na yanayouza bidhaa za LG Tanzania nzima.
Mteja aliponunua kifaa chochote cha picha na sauti kutoka LG alitakiwa kupewa dhamana (warrant) ya miaka miwili na kupewa ticketi ya kujiunga na promosheni hii.
Garnet Star Limited, Wakala mkuu aliyedhibitishwa chini Tanzania.
Tunapenda kuwafahamisha Watanzania kwa ujumla kuwa Promosheni iliyokuwa inaendeshwa na Garnet Star Ltd imekamilika. Kwa maana hiyo Garnet Star limited inatoa pongezi za dhati kwa wateja wao waliofanya manunuzi katika vituo vyao mbalimbali na kupata nafasi ya kujaza kupon za bahati nasibu.
Tunatoa pongezi kwa wateja wafuatao ambao wamejishindia zawadi mbalimbali kama ilivyoorodheshwa:
1. DANIEL V.CHUWA ameshinda TV INCH 55,ULTRA HD
2. SAMWEL TUNGARAZA ameshinda TV INCH 32
3. JOSEPH MUHOZI ameshinda Music System ya model CM9730
4. ABDULIKADRI YUSUPH ameshinda Mobile Photo Printer 
5. DR. ELIAUSOWY MEENA ameshinda Mobile Photo Printer
6. LUGANO JEGELA ameshinda Mobile Photo Printer
7. SAMWEL ameshinda Mobile Photo Printer
8. HAJI MLENDELA ameshinda Mobile Photo Printer
Vyote hivi ni kutoka LG – Garnet Star na vina dhamana (warrant) ya miaka miwili.Tunawakaribisha wateja wote na Watanzania wote kutembelea mawakala wetu mbalimbali waliopo kote nchini na kutembelea ofisi zetu zilizopo jengo la red cross makutano ya Bibi Titi na Morogoro Road ghorofa la tano kwa mahitaji yao yoyote.Nunua bidhaa za LG nawe ufaidike.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...