Wednesday, August 20, 2014

Jeshi la Wananchi wa Tanzania -JWTZ Wazindua Rasmi Wiki ya Jamii kwa Kutoa Msaada wa Vyakula


Mkurugenzi   wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  Brigedia Jenerali Sarah Wambali akisoma risala ya kumkamribisha Mgeni rasmi katika hafla ya kusherekea miaka 50 ya Jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam, ambapo wanatarajia  kutoa misaada ya vyakula na vifaaa mbalimbali  kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

 Mkurugenzi wa Jinsia  kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi ambaye ni mgeni rasmi katika  hafla  ya kusherekea miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania  jijini Dar es Salaam  na kuzindua wiki ya kusaidia jamii kwa kutoa msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

 Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi  kushoto, akikabidhi msaada wa chumvi na baadhi  vyakula kwa  watoto wa kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani cha Mburahati ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi wiki ya huduma kwa Jamii inayoendeshwa na Jeshi la Wananchi  wa Tanzania  jijini Dar es Salaam viwanja vya Lugalo, kulia ni Mkuu wa Utumishi wa Jeshi hilo Meja Jenerali Vincent Mritaba na Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii  Brigedia Jenerali Sarah Wambali.

Mkurugenzi   wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Sarah Wambali akisalimiana na watoto wa kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani cha Mburahati  baada ya kuwakabidhi msaada ya vyakula katikati ni mgeni rasmi Mkurugenzi wa Jinsia  kutoka Wizara ya Maendeleao ya Jamii ,Jinsia na Watoto Meshack Ndasikoi na  kulia ni Mkuu wa Utumishi wa Jeshi hilo Meja Jenerali Vincent Mritaba jijini Dar es Salaam.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...