Kikundi cha Platinum Dancers kikionyesha umahiri wao wakati wa shindano la kumsaka mshindi wa dansi la Serengeti fiesta, lililofanyika katika Ukumbi wa Klabu Lavida , mjini Tanga leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha la Serengeti fiesta linalotarajiwa kufanyika leo jumamosi Agosti 23 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
Majaji wa shindano la kumsaka mshindi wa dansi la Serengeti fiesta wakifuatilia kwa makini namna wasanii wanavyotoana jasho ili kumpata mshindi wa shindano hilo.
Kundi la Street Color, likionyesha umahiri wao katika kinyang’anyiro hicho ambacho mshindi aliondoka na kitita cha sh milioni moja na kupata nafasi ya kutoa shoo katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Lucas Kaili wa kundi la Ice Cream naje akijaribu bahati yake wakati wa shindano hilo.
Kundi la Ice Cream likipozi kwa picha mara baada ya kutangazwa washindi wa dansi la Serengeti fiesta na kujishindia zawadi ya sh milioni moja.
No comments:
Post a Comment