Sunday, January 31, 2010

President Kikwete in Davos


President Jakaya Mrisho Kikwete(right) in conmversation with Vietnam Prime Minister Nguyen Tan Dung(centre) and the chariman of the New Delhi Television Roy Prannoy(left) who was also the moderator during the debate on Global Food Security held at Davos Congress Hall yesterday evening(photos by Freddy Maro)

President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the the Microsoft founder and Chaiman of the Bill and Melinda Gates Foundation, Bill Gates shortly after participating in a debate on improving Food Security held in at Davos Congress Hall, yesterday afternoon.

President Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a debate on improving agriculture production to boost food Security during the World Economic forum in Davos yesterday.On the left is Ellen Kullman Chair and CEO of of the US based DuPont company and on the right is Microsoft  Founder and Chairman Bill Gates.

mambo ya Kipanya

Jerry Muro matatani



HARAKATI za Mwanahabari Bora wa Jumla wa Mwaka 2009 Tanzania, Jerry Muro, za kupambana na kero ya rushwa na ufisadi jana zilimwingiza mwandishi huyo mikononi mwa jeshi la Polisi akituhumiwa kuomba na kupokea rushwa.

Muro, ambaye alikuwa mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV na baadaye kuhamia kituo cha televisheni cha Taifa(TBC1), alikumbwa na mkasa huo leo majira ya saa sita mchana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Sea Cliff.


Akizungumzia suala hilo Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kuwa ni kweli mwandishi huyo amekamatwa na yuko polisi kwa mahojiano.

"Ni kweli yuko hapa na anahojiwa na mimi ndo ninapewa taarifa hivyo nitatoa taarifa kamili kesho saa sita,"alisema Kova.

"Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata, Muro alikamatwa kufuatia mtego uliowekwa na askari polisi mara baada ya kuarifiwa na mfanyabiashara mmoja (jina tunalihifadhi) ambaye ndiye aliyetakiwa kutoa fedha hizo."

Bila kufafanua kwa undani sababu za Muro kutaka kupewa fedha hizo, taarifa zinadai kuwa Muro alikamatwa muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha hizo

“Muro alikuwa ameahidiana na mfanyabiashara ...., ili ampe Sh10milioni kama hongo, lakini mfanyabiashara huyo alitoa taarifa kwa Polisi na ndio leo (jana) wamefanikiwa kumkamata. Walimkamata mara baada ya kupokea fedha hizo,” alisema mtoa taarifa.

Mambo ya twanga







Twanga Pepeta wakiamua kufanya mambo wanafanya kweli hebu wacheki hapa, yaani hapatoshi wakiwa katika harakati zao kwenye ukumbi wakifanya vitu vyao hakika mwenye kuburudika anaburudika si mchezo swali linabadi jeee hawa wasanii wanakipata kile wanachokitaka, wanachokifanya ndicho mnachokitaka, mbona hawa wasanii wa kiume wamevaa vizuri kuliko wa kike au ndo tusemeeeee kazi kwenu.

Friday, January 29, 2010

Mkenya ainusa Man City



KIUNGO wa Kenya, McDonald Mariga anakaribia kuwa Mkenya wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya England baada ya klabu ya Manchester City kuamua kumnunua kutokana na juhudi zao za kumpata Fernando Gago wa Real Madrid kugonga mwamba.
Inter Milan pia imekuwa ikimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya anayechezea Parma ya Italia, lakini inaonekana imeamua kuachana naye baada ya kumpata Manuel Fernando kwa mkopo kutoka Valencia.
Gazeti la Daily Mail limeripoti jana kuwa Man City iko tayari kulipa kitita cha Pauni 6 milioni kumnunua Mariga na inaweza inaweza kumuachia Valeri Bojinov ikiwa ni sehemu ya mpango huo.
Kocha Harry Redknapp alijaribu kumnunua Mariga kutoka klabu ya Helsingborgs ya Sweden wakati akifundisha Portsmouth miaka mitatu iliyopita, lakini kibali cha kazi kilimkwamisha.
Lakini hivi sasa kiungo huyo wa Parma amejichimbia kwenye kikosi cha kwanza, akivutia mashabiki wengi tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2007.

Dk Shein ziarani Kenya



Mhandisi Mkuu wa Kituo cha kuzalisha umeme Mombasa Kenya Peter Onail kulia, akimueza jambo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein, wakati alipotembelea katika kituo hicho kuangali shuhuli za kiutendaji jana. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kenya Dk. Kalonzo Musyoka.

LEO NI LEO JIJINI KAMPALA:R.KELLY IS IN TOWN


Mashabiki wa muziki,hususani wa R&B waliopo katika ukanda wa Afrika Mashariki na hususani jijini Kampala nchini Uganda,huenda leo wakashuhudia onyesho ambalo hawajashuhudia ndani ya miaka kadhaa na huenda wasishuhudie katika miaka kadhaa ijayo.Hiyo ni ahadi,sio kutoka kwa bongocelebrity bali kutoka kwa mwanamuziki Robert Sylvester Kelly maarufu kama R.Kelly(pichani) kutoka nchini Marekani anayetarajiwa kufanya onyesho la aina yake hapo leo jijini Kampala katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval.


Onyesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Zain,limepewa jina la “I Believe”.Hivi karibuni iliarifiwa kwamba kampuni ya Zain imetumbukiza zaidi ya $2.5 kwa ajili ya onyesho hilo kwani inasemekana kwamba kwa R.Kelly kukubali kufanya show yoyote nje ya Amerika Kaskazini basi $600,000 lazima ziwe mezani. Viingilio katika onyesho hilo ambalo tiketi zake zilishakwisha(sold out) wiki mbili zilizopita, vimepangwa kuwa Ushs 30,000(Silver) Ushs 125,000(Gold) na Ushs 250,000(Platinum). Hii ni mara ya kwanza kwa R.Kelly kufanya concert katika ukanda wa Afrika Mashariki. Na barani Afrika kwa ujumla mahali pengine ambapo amewahi kufanya onyesho ni Afrika Kusini tu.


R.Kelly ameahidi kuimba nyimbo zake zote ambazo amewahi kutamba nazo kama vile Bump n’Grind, I Believe I Can Fly,Gotham City,Ignition(Remix),The World’s Greatest,If I could turn back the hands of time, na nyinginezo tele bila kusahau hip-hopera yake ya Trapped In A Closet.

Sasa kwa wale ambao mmeshawahi kuhudhuria show yeyote ya R.Kelly,mnajua kwamba yeye hupenda mashabiki wanaokwenda naye sambamba.Hupenda kuwashirikisha hadhira(audience).Kazi kwenu.Jukwaani R.Kelly anatarajia kusindikizwa na wasanii wa Uganda Bebe Cool,Jose Chameleon,GNL,Peter Miles na Goodlyf ambao ni Radio na Weasel.Wote hao wamepigiwa kura na waganda wenyewe ili kupata nafasi hiyo. Pata uhondo zaidi PIGA CHABO BONGO CELEBRITY ILIKOTOKA TAARIFA HII

JK in davos, switzealand for world economic summit


President Jakaya Mrisho Kikwete in private talks with former US President Bill Clinton in Davos Switzerland. President Kikwete arrived in Davos yesterday to attend the World Economic Forum Summit. Photo by Freddy Maro.

Thursday, January 28, 2010

Aliyedaiwa kufa na kuzikwa aibuka hai



MKAZI wa mjini Mafinga ambaye alidaiwa kufa na kuzikwa mwezi Oktoba mwaka jana, amerejea kwao akiwa hai na kusema “sikumbuki kama niliwahi kufa”.
Kijana huyo, Nickson Kabonge, 23, aliwasili nyumbani kwao juzi mchana akitokea msitu wa Kihanga ulio Mafinga ambako amedai alikuwa akifanya shughuli za kupakia mbao na magogo kwenye magari.
Wakati familia yake, na hasa baba ikiamini kuwa alishafariki na ilishiriki kumzika, kijana huyo aliiambia Mwananchi kuwa aliamua kurejea kwao baada ya kuota kila mara kuwa baba yake amefariki.
Kurejea kwa kijana huyo kulizua yaharuki kwa wakazi wa mjini hapa ambao walifurika nyumbani kwao kumshangaa, wakionekana kutoamini kuwa aliyerejea ni kijana waliyemzika na badala yake kumchukulia kuwa ni msukule.
Pamoja na kurejea kwao, baba wa kijana huyo, Boniface Kabonge alisema kuwa mwanaye Nickson alifariki dunia Oktoba 6 mwaka jana na kuzikwa kwenye makaburi ya Mufindi.
“Nilishtuka mwanangu alipobisha hodi na kuingia ndani wakati najua alishakufa na tulimzika, sijui imekuwaje hadi aliyekufa arejee nyumbani,” alisema
Alisema kabla ya kifo chake kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya kupasua mbao kwenye msitu huo wa Kihanga, lakini alifariki baada ya kuangukiwa na gogo ambalo lilimjeruhi vibaya kichwani.
Alisema mwili wa kijana huyo ulipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi na
kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hadi siku ya pili ulipopelekwa nyumbani
kwao kwa ajili ya kuagwa.
“Mimi ndiye niliyemuosha mwanangu kutokana na mila zetu, tulimpeleka nyumbani watu waliaga kama kawaida na baadaye tulimzika kwa sababu kila mmoja alijiridhisha na kifo chake,” alisema
Akizungumza na Mwananchi kijana huyo alisema hafahamu habari za kifo chake.
“Nashangaa wanaponikimbia ila sikumbuki kama niliwahi kufa, nachojua nilikuwa nikiishi na wenzangu kumi katika msitu wa Kihanga ambako tulikuwa tukila pumba na maji,” alisema
Alisema kuwa kilichomrejesha nyumbani kwao ni ndoto alizokuwa akiota kuwa baba yake amefariki hali iliyomlazimu arudi kuhani msiba.
“Kila nikikaa mwili wa baba yangu ulikuwa ukipita mbele yangu kwenye jeneza huku ukiwa umefunikwa kitambaa chekundu, ndio maana nikaamua kuja kumzika. Nashangaa nilipofika hapa nikaambiwa kuwa mimi ndio nilikuwa nimekufa,” alisema. Tumaini Msowoya, Mufindi

Mwili wa Afisa wa CCM wapokewa


Katibu Mkuu wa CCM, Yussufu Makamba akiwa katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere na ndugu wa aliyekuwa afisa wa kitengo cha maadili na Usalama cha chama hicho, Yoaza Mjema leo mchana Yoaza alifariki dunia nchini India alikokwenda kwa matibabu, maziko ya Mjema yanafanyika Tanga.

Dk Njelekela apata tuzo ya Martin Luther King



MWENYEKITI wa Chama cha Madaktari Wanawake (Mewata), Dk Marina Njelekela amepewa tuzo ya amani ya Dk Martin Luther King l kutokana na kuendesha kwa mafanikio kamapeni ya kupima na kutibu saratani ya matiti na uzazi bure.
Akitoa tuzo hiyo ya 2010 Martin Luther King Jr./ Drum Major for Justice jana kwenye ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, Balozi Alfonso E Lenhart alisema Dk Njelekela amepata tuzo hiyo kutokana na kupigania utu wa mwanamke kwa kuendesha kampeni hiyo na kuokoa maisha ya kina mama wengi nchini bila kujali kipato chao, elimu wala mahali wanapoishi.
Alisema Dk Njelejela aliafanya kazi kubwa sana kwa kuwa kati ya wanawake 1000 wanaojifungua nchini, sita kati yao hufariki.
Alisema mchango alioutoa Dk Njelekela ulilenga kuweka usawa na utu kwa wanawake, na kuwa hilo ndilo lililokuwa lengo la Dk Martin Luther King, ambaye alikuwa mpigania haki za wanyonge na hasa watu weusi nchini Marekani.
Alisema Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kama Mewata katika kuchangia sekta ya afya nchini ili kuhakikisha kuwa watu wote bila kujali hali zao za kipato, elimu, wala mahali wanapoishi wanapata huduma bora na sawa za afya.
Akizungumza baada ya kuipokea tuzo hiyo, Dk Njelekela, ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (Muhas), aliishukuru Marekani kwa kutambua mchango wake na kumpatia tuzo hiyo ya amani na kuwataka madaktari nchini kuchukulia tuzo hiyo kama changamoto ya kupigania kuinua na kuboresha afya nchini.
“Kampeni hii kupima na kutibu saratani ya matiti na shingo ya uzazi tuliifanya katika mikoa saba, mimi na wenzangu wa mewata tuliwafikia wanawake kama 64,000,” alisema Dk Njelekela.
Dk Njelekela pia alitumia nafasi hiyo kuiomba Marekani kuiunganisha Mewata na madaktari wengine wa nchi hiyo ili waweze kuendelea kutoa huduma za afya kwa Watanzania.
Mbali na Dk Njelekela watu wengine ambao walishapata tuzo hiyo ni pamoja na Joseph Sinde Warioba (1999), Mwalimu Julius Nyerere (2000), Francis Nyalali (2002), Profesa Godfrey R.V. Mmari (2003) Mama Justa Mwaituka (2004), Balozi Gertrude Mongella (2005), Dk Salim Ahmed Salim (2006), Rashid Mfaume Kawawa (2007), Regnad Abraham Mengi (2008) na jumuiya ya maalibino Tanzania (2009). Imeandikwa na Fredy Azzah.

Wednesday, January 27, 2010

Wanajeshi wanaodaiwa kumuua mtoto wa Fundikira kizimbani



ASKARI wawili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za mauaji ya mtoto wa mwanasiasa maarufu, Chifu Abdallah Fundikira.

Watu hao, Rhoda Robert, 42, wa cheo cha sajenti mwenye namba MTM 1900 kutoka kambi ya JKT Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe, 37, wa kambi ya JWTZ Kunduchi, wanakabiliwa na mashtaka ya kumuua Swetu Fundikira, 45.

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Geni-Vitus Dudu, wakili wa serikali, Monica Mbogo alidai kuwa washtakiwa walifanya mauaji hayo Januari 23, mwaka huu, majira ya saa 7:30 usiku kwenye Barabara ya Mwinjuma wilayani Kinondoni.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu shtaka hilo linalowakabili ni moja ya mashtaka ambayo Mahakama ya Kisutu haina uwezo wa kuyasikiliza bali Mahakama Kuu.

Hakimu Dudu aliamuru askari hao walirudishwe rumande kwa kuwa shtaka hilo lao halina dhamana na akaiahirisha kesi hiyo hadi Februari 10 itakapotajwa tena baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi bado haujakamilika.

Askari hao wanadaiwa kumuua Swetu kwa kumpiga wakiwa pamoja na mwanajeshi mwingine mmoja baada ya kutokea ugomvi wa barabarani uliotokana na askari hao kudai kuwa walifanyiwa fujo na kutukanwa.

Swetu alifariki dunia Jumapili usiku akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kipigo hicho. Imeandikwa na Tausi Ally

Moto waunguza tena Bagamoyo





MOTO mkubwa umeteketeza, soko, vibanda vya kukaangia samaki na migawaha zaidi ya 40 katika eneo la bandarini mjini Bagamoyo.
Moto huo umewatonesha kidonda wakazi wa Bagamoyo ambao mwaka jana, walikumbwa na balaa la kuteketea kwa hoteli ya Paradise, moja ya miundombinu muhimu ya uchumi wa eneo hilo.
Jana majira ya saa 9:30 jioni moto mwingine mkubwa ulilipuka katika vibanda hivyo na hakukuwa na kikosi chochote cha Zimamoto kilichofika eneo hilo kuuzima hadi saa 10:00 gazeti hili lilipoondoka eneo la tukio.
"Hivi unavyoona vinaungua ni vibanda vya wakaanga samaki, pale kuna migahawa ya chai kwa ajili ya wavuvi wanaotia nanga wakitoka baharini," alifafanua mvuvi mmoja ambaye kwa wakati huo hakuwa tayari kutaja jina lake.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magesa Mulongo, alipotafutwa kwa njia ya simu kutoa taarifa kamili ya hasara, simu yake hiyo ya kiganjani iliita bila majibu kama ilivyokuwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoani humo Absolom Mwakiyomo, ambaye naye hakupokea simu.
Lakini, kwa mujibu wa Mvuvi huyo, moto huo ulipata msukumo mkubwa kutokana na upepo maarufu kama Kaskazi ambao mara nyingi huvuma kutoka Pwani kwenda Bara.
"Kwakweli wavuvi na wamiliki wa migahawa hii wamepata hasara kubwa kweli, hili ni eneo lao muhimu kiuchumi, kuungua kwa migawaha kutarudisha nyuma kasi ya shughuli za uchumi," alielezea tukio hilo ambalo gazeti hili imefanikiwa kupata picha za moja ya kibanda kilichokuwa kikiteketea.
Eneo hilo ni maarufu kwa wavuvi ambao hutia nanga kwa ajili ya kuuza samaki wao kwa wafanyabiashara mbalimbali ambao nao hukaanga na kuuza kwa wateja wengine mbalimbali.
Gazeti hili lililokuwepo eneo la tukio lilishuhudia moto huo ukitekeleza vibanda hivyo huku wamiliki wake wakijitahidi kuuzima bila mafanikio.
Uchunguzi wa awali wa Mwananchi, umebaini kwamba chanzo cha moto huo kilitoka ndani ya moja ya kibanda kati ya vilivyoungua eneo hilo la tukio. Imeandikwa na Christopher Buke.

Tuesday, January 26, 2010

Maandalizi tamasha la busara


Mwanamziki wa Kitanzania anayeishi nchi Japani, Fresh Jumbe akizungumza wakati wa mkutno na waandishi jijini Dar es Salaam jana kuhusu ushiriki wake katika tamasha la saba la muziki wa Sauti za Busara linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao katika Ngome kongwe mjini Zanzibar. Picha na Salhim Shao

Monday, January 25, 2010

Kituo cha Ubungo leo hii


Picha iliyopigwa kutoka juu ikionyesha kituo cha kidogo cha daladala Ubungo (Minazi - old name). Hapo awali daladala zilikuwa hazilipii kuingia ama kutoka. Kwa sasa manispaa imeanza kuwatoza kila wanapotoka katika lango kuu la kituo

Sunday, January 24, 2010

’ Nuru the Light’




Msanii wa muziki wa kizazi kipya,’ Nuru the Light’ (kushoto) pamoja na wasanii wa Kundi la THT wakishambulia jukwaa wakati wa uzinduzi wa albamu yake kwenye Ukumbi wa Florida jijini Dar es Salaam juzi.

Vodacom yazindua RED ALERT kuchangia maafa



Kampuni ya simu za mkonini Ya Vodacom Tanzania leo imezindua kampeni maalum ya kuchangia waliopatwa na maafa nchini, Kampebni ijulikanayo kwa jina la VODAFONE RED ALERT. Pichani ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bakari Shabani akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Dietlof Mare wakizindua huduma jhiyo pamoja na viongozi wa Vodacom kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno unaotozwa Sh 250.

kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanziar leo


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Zanzibar Mhe.Amani Abeid Karume na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wakipiti makabrasha ya ajenda mbalimbali, kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui mjini Zanzibar leo.



Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Amani Abeid Karume, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamaed Shein katikati, Rais Mstaafu Mzee Ali Hassani Mwinyi kulia, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha kushoto na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Saleh Ramadhani Feruzi wa pili kushoto wakikiingia katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kuanza kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanziar leo.

Amour Nassor (VPO)

waasisi wa CCJ



Katibu wa CCJ, Renatus Muabhi (mwenye shati la kijani) na Mwenyekiti Richard Kiyabo (mwenye shati la cream).

SIKU nne baada ya Msajili wa vyama vya Siasa John Tendwa kutoa usajili wa muda kwa Çhama Cha Jamii (CCJ) kinachohusishwa na vigogo wa CCM, chama hicho kimesema kitasimamisha mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wa muda wa chama hicho, Richard Kiyabo aliliambia Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalum kuwa jana kuwa kuwa na mgombea wa urais katika uchaguzi huo ndilo lengo lao la msingi kusajili chama hicho sasa.
Alisema mbali na kumsimamisha mgombea urais, CCJ inajipanga kusimamisha wagombea wa ubunge katika majimbo yote ya Tanzania bara na visiwani.
“Hilo ndilo lengo letu kubwa kuwa na mgombea urais, tutasimamisha pia wagombea katika majimbo yote bara na visiwani. Tunao wanachama hadi Zanzibar,” alisema Kiyabo alipoulizwa kama wana mpango wa kumsimamisha mgombea urais katika uchaguzi ujao.
Hatua hiyo ya CCJ inaonyesha wazi kuwa sasa mgombea wa chama hicho atapambana na Rais jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao kama atapitishwa na chama chake kuwania urais katika ngwe ya pili.
Kiyabo alisema CCJ imeanzishwa kuziba pengo la upinzani ambao sasa unaonekana kulegalega baada ya vyama vilivyopo kupoteza mwelekeo.
“Hakuna vyama vya upinzani vyenye nguvu nchini, wapinzani wamekalia kumsifia Rais Kikwete. Sisi tunadhamiria kuonyesha sera mpya zitakazoleta changamoto. Tunataka Watanzania wafurahie matunda ya rasilimali za nchi yao na pia wawe na uhuru wa kujitafutia maendeleo,”alisema.
Kiyabo ambaye ana taaluma ya Sayansi ya Jamii alisita kuwataja wadhamini wa chama hicho akieleza kuwa ni mapema mno kufanya hivyo sasa, ingawa baadhi ya vigogo wakubwa ndani ya CCM hususan ambao hawaridhishwi na mwenendo ndani ya chama hicho wanadaiwa kuwa wapo nyuma yake.
“Ukifika wakati wake tutawatajia, ila kwa sasa tunasisitiza kwamba hiki ni chama kilichoanzishwa na wananchi wenyewe.”alisema.
Hata hivyo, Katibu wa uenezi na itikadi wa CCM, John Chiligati alinukuriwa juzi akisema kuwa chama chao hakihofii usajili wa CCJ, ambacho kinahusishwa na baadhi ya vigogo wa chama tawala na upinzani, wakiwemo wabunge.
Alisema CCM bado ni imara na haiwezi kutikiswa na kuanzishwa kwa CCJ kwa kuwa haina ubavu wa kuimega CCM.

Chiligati alisema CCM imepokea taarifa za kuanzishwa kwa CCJ kama ilivyopokea taarifa za usajili wa vyama vingine vya siasa kwa kuwa uanzishwaji wake uko katika utaratibu wa sheria.

Mwenyekiti CCJ alitamba kwamba hadi kufikia mwishoni mwa Februari mwaka huu, watakuwa wamekamilisha masharti ya msajili wa vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na kuwa na wanachama 200 katika mikoa minane bara na mikoa miwili visiwani.
“Tutahakikisha tunakamilisha masharti ya msajili wa vyama vya siasa kabla ya kwisha Februari. Tumejiandaa vya kutosha hadi sasa tuna wanachama 2000 hapa jijini Dar es Salaam na pia tunao wanachama wengi mikoani,”alisema.
Naye Katibu wa muda wa chama hicho, Renatus Muabhi alisema CCJ kimeanzishwa kuleta mapinduzi ya kisiasa na kiuchumi miongoni mwa jamii ya watanzania na sio kuigawa CCM.Picha na habari za Elias Msuya na Sadick Mtulya.

President Kikwete visit U.S. Navy ships

President Jakaya Kikwete onboard USS Nicholas with Commodore Mark Kesselring, accompanied by U.S. Ambassador Alfonso Lenhardt (background, left). President Kikwete visited the ships USS Nicholas and US Navy's high speed vessel Swift on January 23, 2010. The two U.S. Navy ships are in Tanzania to participate in maritime and cultural exchanges
with the Tanzanian Navy. The vessels are visiting ports in Djibouti, Kenya, Tanzania, Mozambique, Mauritius, Seychelles and Comoros to enhance maritime safety and security in the region. (Photo Courtesy of the U.S. Embassy)



Kamanda anayeingoza meli ya kivita ya jeshi la Marekani Mark Kesselring akimuongoza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kukagua meli hiyo USS Nicholas wakati Rais Kikwete alipoitembelea meli hiyo na kuzungumza na maofisa wa kijeshi wailomo katika meli hiyo leo jioni katika bandari ya Dar es Salaam.

Saturday, January 23, 2010

Wawakilishi Zanzibar


Spika wa baraza la wawakilishi, Pandu Ameir Kificho akisalimiana na mwakilishi wa viti maalum wanawake CUF, Zakia Omar. kulia ni mwakilishi wa Bububu, Khatibu Suleiman bakari nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi.

Kumekuwa na udhaifu katika kutunza mazingira yanayobeba vivutio vya utalii katika mji mkongwe wa Zanzibar kama picha inavyoonyesha kaburi la mfanyabiashara maarufu wa enzi hizo, Tiptip lilivyoachanizwa na sehemu hiyo baadhi ya watu wamefanya dampo la takataka ambapo watalii wengi baada ya kutembelea nyumba yake Shangani pia huzuru kwenye kaburi hilo.

Waziri wa katiba na utawala bora, Ramadhan Abdalla Shaaban (kushoto) akibadilishana mawazo na mwakilishi wa Ole, Hamad Omar Masoud (kati) na Assaa Othman Hamad wa Wete nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi jana. picha zote na Martin Kabemba.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wakifurahia jambo baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi. kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi na wawakilishi wa CUF, Juma Haji Duni na Nassor Ahmed Mazrui jana.

Wednesday, January 20, 2010

LILIAN MDUDA ATINGA FAINALI ZA "FACE OF AFRICA" LAGOS NIGERIA!!



Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa habari kweye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es salaam leo wakati akitoa taarifa juu ya mshiriki wa Mnet Face of Africa Lilian Mduda ambaye yuko naye pichani kutoka Tanzania kutinga katika fainali za shindano hilo zitakazofanyika nchini Nigeria katika jiji la Lagos Februari 6/ 2010 ambapo washiriki 10 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye fainali hizo watachuana.
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikipeleka wawakilishi mara kwa mara katika shindano hilo kubwa la uanamitindo katika bara la Afrika,
Kwa Tanzania mwanamitindo Miriam Odemba ndiye aliyewahi kushika nafasi za juu katika shindano hilo akiwakilisha Tanzania miaka ya nyuma na alifanikiwa kuingia mkataba wa kufanya kazi za uanamitindo na kampuni ya Elite Model Look ya Afrika Kusini.
Hata hivyo kampuni hiyo ilikatisha mkataba na Miriam Odemba na kumrejesha nyumbani baada ya mwanamitindo huyo kushindwa kufuata maelekezo ya kitaalamu aliyokuwa akipewa na wakuu wake katika kampuni hiyo ambapo inadaiwa alishindwa kufuata mpangilio mzuri wa kula chakula na mazoezi kitu kilichomfanya anenepe na kushindwa kukidhi viwango vya uanamitindo vilivyokuwa vikitakiwa na kampuni hiyo.
Mwakilishi wa mwaka huu Lilian Mduda ambaye ni mwanfunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam amesema amejiandaa vyema kwa ajili ya shindano hilo na haoni mshiriki yeyote anayemtisha isipokuwa ni yeye mwenyewe anayeweza kujiwekea mazingira ya kushinda kwa kuzingatia yale yote atakayoelekezwa na kuyafanya kwa ufanisi ili aweze kufikia malengo yake katika fainali hizo

Wasanii watumbuiza Bagamoyo



Wasanii wa kikundi cha Chibite wakitumbuiza katika mkutano kati ya Waziri Mkuu na Madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo na viongozi wa wilaya hiyo, mjini humo Januari 20, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Kikwete afungua daraja la Mto Simiyu


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria kufungu rasmi daraja la Mto Simiyu,lililopo kati ya mpaka wa wilaya za Bariadi na Meatu,mkoa wa Shinyanga jana asubuhi.

Mbunge wa Bariadi Mashariki John Momose Cheyo(kulia), Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (kushoto pembeni ya Rais) pamoja na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali wakishangilia mara baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi daraja la mto Simiyu lililopo katika mpaka wa wilaya za Meatu na Bariadi mkoani Shinyanga jana mchana.Wanne kushoto ni Mama Salma Kikwete.(picha na Freddy Maro)

Tuesday, January 19, 2010

Msafara wa Rais wapata ajali

GARI la polisi lililoongoza msafara wa Rais Jakaya Kikwete aliyepo mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ya siku tatu jana hiyo liliacha njia na kupinduka na kujeruhi askari.

Walioshuhudia ajali hiyo walisema waliliona gari hilo lililokuwa mbele ya msafara wa rais likiyumba na baadaye kuacha njia na kupinduka kando ya barabara iendayo Meatu. Ajali hiyo ilitokea saa 11 na dakika kumi jioni.

Katika ajali hiyo askari sita walijeruhiwa na ilitokea katika kijiji cha Nyikoboko wakati msafara ukitokea Kisese wakati Rais Kikwete akitoka kuzindua mto Simiyu unaounganisha Wilaya za Bariadi na Meatu.

Walioshuhudia walisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na mvua zilizonyesha na kusababisha utelezi hali iliyosababisha gari la polisi lenye nambari za usajili PT 7414 kuacha njia na askari wawili kujeruhiwa ambao ni Marko Mbambwe na DC Tegemeo. Meya wa mji wa Shinyanga Hassan Mwendapole alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Majeruhi hao wapo katika hospitali ya Wilaya ya Meatu na kwamba katika ajali hiyo gari aina ya Suzuki ambayo ilikuwa karibu na gari iliyopata ajali iligongana na gari iliyokuwa nyuma.

Ajali juu ya ajali


Wakazi wa eneo la Tabata Kisiwani jijini Dar es Salaam, wakichukua mafuta ya petroli kutoka katika roli lililopata ajali katika barabara ya Mandela. Picha na Michael Matemanga.

Tanzania Diaspora



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifungua mkutano wa wadau wa majadiliano baina ya wataalamu wa hapa nyumbani na wa nje jijini leo kuhusu uwezekano wa kuwashirikisha kikamilifu Watanzania walio nje ya nchi mkutano huo unaratibiwa na Wizara ya Nje ambayo tayari wameshaunda Idara ya DIASPORA.
(Picha na Mwanakombo Jumaa -MAELEZO).

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...