Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na
wafanyakazi wa Mkoa wa Mbeya alipokagua jingo la kitega uchumi la Lupa Way
Jijini Mbeya ambalo pia litakuwa na Ofisi za NHC Mkoa wa Mbeya.
Thursday, August 13, 2015
ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC KATIKA MIKOA YA MTWARA, RUVUMA, NJOMBE NA MBEYA KUKAGUA MIRADI
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake
akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika
hilo eneo la Napupa Mjini Masasi.
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Paul Mkami(kushoto)
akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake
ramani ya eneo la ardhi lililopewa NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama
nafuu Wilayani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake
wakitembelea eneo la kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Namtumbo
alipofanya ziara yake katika Mkoa wa Ruvuma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake
wakikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa Ofisi ya Shirika Mkoani Ruvuma
ambapo ameagiza Ofisi hiyo iwe imekamilika ndani ya mwezi mmoja ili kuwapa
fursa wateja na wananchi kupata huduma kwa urahisi. Kwa muda mrefu NHC haikuwa
na Ofisi ya kudumu katika Mkoa wa Ruvuma kutokana na shughuli za Mkoa huo
kusimamiwa na Mkoa wa NHC wa Iringa.
Mradi wa nyumba za gharama nafuu unaojengwa na NHC Wilayani Makete nao
ulipata fursa ya kutembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando
Mchechu na ujumbe wake. Hapa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa Bw.
Raymond Mndolwa anaonyesha eneo ambalo litajengwa Kituo cha biashara ili
kuhudumia wakazi watakaoishi katika
nyumba hizo za kisasa zinazouzwa kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa
Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio juu ya hatua za ukamilishaji wa
mradi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo alipotembelea
mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2015.
Hali ya utekelezaji wa mradi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Busokelo inavyoonekana hivi sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake
wakiukagua mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC Wilayani
Mbarali.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakiwa
na Viongozi wa TRA Mkoa wa Mbeya walipotembelea na kukagua maeneo yanayofaa kwa
uwekezaji wa majengo ya biashara katika Mpaka wa Tanzania na Zambia –Tunduma.
Taratibu zikikamilika NHC itajenga jingo la biashara katika mpaka huo maarufu
na muhimu kiuchumi. Picha zote na Muungano Saguya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma
Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment