Monday, August 10, 2015

SEMINA YA MPANGO WA KUPUNGUZA VIFO VYA AJALI YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Ofisa Mradi wa mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani unaosimamiwa kwa kushirikiana na  Bloomberg (BIGRS), Shirika la afya Duniani (WHO)  na Serikali ya Tanzania, Mary Kessi (katikati), akitoa mada kwenye semina hiyo iliyowajumuisha wanahabari na wadau wa sekta ya usafiri inayohusu  mpango huo wa utekelezaji wa mkakati huo.
 Mtaalamu Mwelekezi, Callie Long kutoka Canada akitoa mada kwenye semina hiyo. 
 Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Asah Mwambene akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi Sokoni Deus (katikati), akitoa mada kwenye semina ya siku mbili ya wanahabari na wadau wa sekta ya usafiri Dar es Salaam leo asubuhi, inayohusu  mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye 
semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mmoja wa wadau wa semina hiyo akichangia jambo.
……………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
Mradi wa usalama barabarani kwa kushirikiana na  Bloomberg (BIGRS), Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa  umeanza kutoa mafunzo kdau wa sekta wa usafiri wakiwemo wanahari, wanasheria kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya ajali.
 
Akizungumza Dar es salaam leo kwenye semina ya siku mbili  inayohusu mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani, Ofisa Mradi huo,  Mary Kessi alisema waandishi wamekuwa wakisubiri matukio ya ajali ndipo waripoti habari hizo jambo ambalo si lazima lisubiriwe na inachotakiwa ni kujenga mazoea ya kuandika habari za kufundisha jamii na watumiaji wa vyombo vya moto namna ya kuweza kuepuka kusababisha ajali.
 
“Dhumuni la semina hii ni kujua jinsi ya kuripoti habari hizi za usalama barabarani ili kufikia walengwa kwa kuongea kupitia vyombo vyenu vya habari ili kuwapa ulewa watu wote’ alisema  Kessi.
 
Alisema kuwa mpango huo wa miaka mitano utaelekeza katika kupunguza ajali za barabarani  huku takwimu zinaonyesha ajali hizo zimekuwa zikiua watu milioni1.24 kila mwaka Duniani, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya taifa huku kati ya hao 20 upata ulemavu kutokana na ajali.
 
Alifafanua kuwa uzembe wa madereva usababisha ajali zinazoweza kuzuilika na kuzitaja sababu hizo kuu ni kutofunga mikanda ,kuendesha gari kwa kasi ,matumizi ya pombe kupita kiwango na kutoweka vizuwizi vya watoto.
 
“Uendeshaji wa gari ukiwa umelewa ni kitu kibaya sana wengine wanaendesha gari huu wanachati na simu bila kujali kilichokua mbele wala nyuma yake”alisema
 
Daktari wa Kitengo cha Maafa na Dharura wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,  Mery Kitambi,alisema Hospitali za mikoa zilizopo nchini hapa zimejaa majeruhu wa ajali pamoja na vifo vinavyo sababishwa na ajali hizo.
 
Alisema waandishi wanatakiwa kuleta fikra mpya kwa  watumia wa vyombo hivyo vya moto ili wajue ni kiasi gani wanajiweka katika hatari na jinsi ya kuepuka hatari hizo.
 
“Ukienda hospitali utawakuta majeruhi wa ajali ni wengi kuliko unavyo fikiria hivyo ni vyema wakajua kwa undani jinsi gani ya kuepuka ajali za kizembe”alisema Kitambi.
 
 
Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi, Sokoni Deus, alisema wazazi wanatakiwa kuacha tabia ya kuwapa watoto walio chini ya miaka 18 kuendesha vyombo vya moto kwani usababisha ajali.

No comments:

Rais Samia Aongoza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma

Dodoma, 18 Januari 2025 – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameo...