Thursday, August 13, 2015

MSAFARA WA LOWASSA WAZUIWA NA POLISI MWANGA, PIA ALIKUWEMO MBATIA N A MREMA, WAKIELEKEA MSIBANI KWA MAREHEMU PETER KISUMO


Msafara wa Mhe.Lowassa wazuiliwa na wananchi mosh wakililia kumuona maeneo ya Boma akitokea KIA kuelekea msibani Mwanga..




NA K-VIS MEDIA, MWANGA
MSAFARA wa mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano kupitia UKAWA Edward Lowassa uliokuwa njiani kuelekea Ugweno Mwanga,  kwenye mazishi ya mwanasiasa mkongwe, Peter Kisumo, umezuiwa na polisi kwenye kijiji cha Maroro leo Agosti 13, 2015.
Kwenye msafara huo pia alikuwemo Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia,Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo.
Kwa mujibu wa waliokuwepo kwenye eneo la tukio, Polisi hao walisema amri kutoka juu zimezuia msafara huo.
Hata juhudi za Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kufanya majadiliano marefu wakuu wa polisi waliokuwepo eneo la tukio, ziligonga mwamba, kuruhusu msafara huo kuendelea na safari yake
Akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye msafara huo,Mbatia alisema kuwa pamoja na kuzungumza na Mkuu wa jeshi la Polisi IGP, Ernest Mangu, lakini mkuu wa Polisi Mwanga alikataa kitii maelekezo yake.
"Nimeongea na IGP akiwa Kibondo,tukakubaliana na kutoa maelekezo kwa RPC,lakini tuliporuhusiwa na kuanza kuondoka, ikaja amri kutoka Kwa OC CID akiwa huko juu msibani ya kwamba hakuna kuruhusu msafara huo, kama kupanda ni gari moja tu ya mh Lowassa na yangu.." Alisema Mbatia na kuongeza.
Lowassa ambaye muda wote alikuwa ametulia kwenye gari pamoja na mzee Ndesamburo,alionekana kukerwa na Hali hiyo.
Polisi wakiwa na silaha pamoja na mabomu ya kutoa machozi, waliweka kizuia cha gari katikati ya barabara ya Moshi-Korogwe. Polisi iliruhusu gari lililombeba Mh. Lowassa na linguine moja gtu ndiyo yapite, agizo lililopingwa vikali


 Mh. Mbatia (kulia), akiwa katika majadiliano na afisa wa polisi Mwanga

Mh. Mrema,(katikati), akiwa na Mh.Joseph Selasini, (kulia)

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...