Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade wakiangalia uzinduzi wa mpango Mkakati wa Chama hicho wa mwaka 2015-2020 uliozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na chama hicho kwenye hoteli ya Hyyat Regency Dar es salaam kutimiza miaka 25 tangu chama hicho kianzishwe hapa nchini, ambapo wanasheria wanawake na waheshimiwa Majaji walialikwa katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regecy Dar es salaam
Mh. Jaji Winnie Korosso akizungumza na wageni waalikwa Wanasheria wanawake wakati wa hafla ya TAWLA ya kutimiza miaka 25 tangu ianzishwe.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Kamishna wa TRA Bw. Rasheed Bade kushoto akijumuika na wageni waalikwa wanasheria wanawake katika hafla hiyo.
Baadhi ya majaji wakiwa katika hafla hiyo.
Waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki kulia akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade, kulia ni Mkurugenzi wa TAWLA Tike Mwambipile.
Bendi ya Skylight ikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade kushoto na Mkurugenzi wa TAWLA Tike Mwambipile wa tatu kutoka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanasheria wa TAWLA.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment