Monday, June 15, 2015

MAMA SALMA KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA WAKE WA MARAIS NA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA HUKO AFRIKA KUSINI.

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Mfalme Mswatti wa Swaziland, muda mfupi kabla ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (AU) unaofanyika  Sandton International Conference Center huko Johanessburg Afrika Kusini tarehe 14.6.2015. Aliyesimama kulia ni Mke wa Rais wa Afrika Kusini Mama Tobeka Madiba Zuma.
2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Antoinette Sessou Nguesso Mke wa Rais Dennis Sessou Nguesso wa Congo Brazaville wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika unaofanyika  Afrika Kusini tarehe 14.6.2015
3
Baadhi ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuhudhuria kikao cha ufunguzi tarehe 14.6.2015. Aliyekaa katikati ni Mke wa Rais wa Congo Brazaville Mama Antoinette Sessou Nguesso na kulia ni Mke wa Rais Afrika Kusini Mama Tobeka Madiba Zuma.
4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Rais wa Congo Brazaville Mama Antoinette Sessou Nguesso kabla ya viongozi hao kuhudhuria sherehe ya ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa AU huko Jahanesburg.
5
Mke wa Rais akisalimiana na Madame Monica Geingob, Mke wa Rais wa Namibia wakati wakisubiri ufunguzi rasmi wa mkutano wa 25 wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika unaofanyika huko Afrika Kusini.
6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Madame Getrude Maseko Mutharika, Mke wa Rais wa Malawi kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Marais na Wakuu wa AU.
7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia Mke wa Rais wa Kenya Mama Magreth Kenyatta wakati wa kikao cha Marais na wakuu wan chi za Afrika.
8
Wake wa Marais wa nchi mbalimbali za Afrika wakibadilishana mawazo kabla ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Marais wa Afrika unaofanyika huko Johannesburg. Waliokaa kutoka kushoto kwenda kulia ni Mama Magreth Kenyatta, Mama Tobeka Madiba Zuma, Mama Salma Kikwete, Mama Antoinette Sessou Nguesso na Mama Hinda  Derby Itno, Mke wa Rais wa Chad na Mwenyekiti wa OAFLA anayemaliza muda wake.
9
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Ghana Lord INA Draman Mahama wakagti wa sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa Marais wa AU unaofanyika Afrka Kusini.
 PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI.

No comments:

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa  Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe ...