Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Kevin Mandopi akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika kwenye ofisi za Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Bibi. Neema Ringo na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bibi. Mary Massay akitoa ufafanuzi kuhusu haki za watu wenye ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwenye mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino leo jijini Dar es Salaam ambapo ameishauri Serikali kuweka mikakati ya muda mrefu ili kukomesha ukatili na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualbino.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Bibi. Neema Ringo (kushoto) akitoa rai kwa watanzania kutoa taarifa mapema za vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Kevin Mandopi na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa masuala ya haki za binadamu wakifuatilia mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Fatma Salum – Maelezo
No comments:
Post a Comment