Mijiolojia wa Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe akizungumzia sekta ya madini nchini kabla ya kumkaribisha Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje ili aweze kufungua mafunzo kwa wataalam wa Wizara. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini na kufanyika Bagamoyo mkoani Pwani, yanatolewa na Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka India, lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu na kuwapa uelewa katika usimamizi wa mazingira kwenye migodi.
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifungua mafunzo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya Nishati na Madini (wa kwanza kushoto, waliokaa mbele) pamoja na washiriki wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka Nchini India (hawapo pichani) katika mafunzo kuhusu usimamizi wa mazingira migodini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya wataalam kutoka Idara ya Madini iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada kuhusu usimamizi wa mazingira kwenye migodi katika nchi ya India iliyokuwa inawasilishwa na mtaalam mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (hayupo pichani) kwenye mafunzo hayo.
Mtaalam kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Srestha Banerjee akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
Mtaalam mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya Nishati na Madini (wa tatu kutoka kushoto, waliokaa mbele), Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Gideon Kasege ( wa pili kutoka kulia, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment