Thursday, May 07, 2015

WAKUNGA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KUTENGENEZA TAIFA LA KESHO

DSC_0228

Rais wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga akimkaribisha Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges (kulia) kuzungumza na wakunga nchini waliokusanyika kwenye mdahalo wa siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Musoma mkoani Mara. Kushoto ni Kaimu Muuguzi mkuu wa serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
DSC_0247
Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges akizungumza na Wakunga nchini Tanzania waliohudhuria kwenye mdahalo wa siku moja uliofanyika kwenye ukumbi wa Mara ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mara mjini Musoma kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga duniani kujadili changamoto zinazowakabili Wakunga nchini. Katikati ni Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy Mwanga na Kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikalim kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala.
DSC_0105
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wakunga nchini waliohudhuria mdahalo huo wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mdahalo huo.

No comments:

WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA KAMPENI YA ‘PERFOM AND INFORM’

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, akizungumza katika Kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika leo Januari ...