Monday, May 25, 2015

JARIDA LA “BANG” LATIMIZA MIAKA KUMI NA MOJA YA UTENDAJI WAKE

ba1
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Relim Entertainment ,Emelda Mwamanga akionyesha  Jarida la Bang!  toleo la 55 ambalo limeadhimisha miaka 11 tokea kuanzishwa kwa jarida hilo.
ba2
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Relim Entertainment ,Emelda Mwamanga akipozi kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya kuongea na wanahabari kwenye sherehe ya kuadhimisha miaka 11 tokea kuanzishwa kwa Jarida la Bang!.
ba3
Keki ya maadhimisho ya miaka 11 ya Jarida la Bang! lenye Cover Page ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu na Mkewe Bi. Faraja Nyalandu
ba4
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Relim Entertainment ,Emelda Mwamanga akiongea na wanahabari wakati wa kuadhimisha miaka 11 tokea kuanzishwa kwa Jarida la Bang!.
ba5
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Relim Entertainment ,Emelda Mwamanga akimlisha keki Mkurugenzi wa Fullshangwe Blog John Bukuku kwa niaba ya wanahabari waliohudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 11 ya toleo la Jarida la Bang!.
ba6
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Relim Entertainment ,Emelda Mwamanga wakionyesha jarida la Bang! na Katibu Muhtasi wake Darliana Mbedule
……………………………………………………………
Naomba nianze kwa kumshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kutukutanisha leo.
Ndugu waandishi wa habari napenda kutumia fursa hii kuwashukuru tena kwa kuitikia wito wetu na kuhudhuria mkutano huu muhimu ambao dhumuni lake kubwa ni kuelezea jarida letu la BANG! lilivyojipanga kuinua na kukuza vipaji vya wanawake nchini katika miaka ijayo.
Jarida la BANG! katika kipindi chote tangu kuanzishwa kwake limekuwa likiandika habari mbalimbali kuhusiana na masuala ya wanawake,vijana na jamii na kuwezesha kuwainua vijana kwa kuvitambulisha vipaji vyao.
Katika kusherehekea miaka kumi na moja jarida letu limejipanga kuhakikisha linajikita zaidi kuinua maisha ya wanawake kwa kuvitambulisha vipaji na biashara zao na kuandika habari mbalimbali zitakazowawezesha kutambulika Afrika yote kwa ujumla. 
Jarida la BANG! limekuwa likisambazwa katika mikoa yote ya Tanzania, Kenya na Uganda. Moja ya mipango mikubwa tunayo iandaa ni kuweza kulisambaza jarida la BANG! katika nchi ya Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia katika kipindi kisichozidi miaka miwili ijayo.
Katika kusherehekea miaka kumi na moja jarida letu pia limekuwa likitambua michango mbalimbali iliyoletwa na viongozi wetu wa kisiasa katika majimbo yao na kutaka katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu jamii iweze kuwatambua viongozi wanaowachagua kwa kuyafahamu maisha yao.
Leo tunasheherekea miaka 11 ya Jarida letu lenye mafanikio makubwa kwenye kazi zetu tukaona ni vyema kumshirikisha Mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu na Mkewe Faraja Nyalandu kwenye toleo hili maalum kuelezea historia ya maisha yao. 
“ Tunawakaribisha viongozi wote wa kisiasa kuonesha ushirikiano wao kwa kuwa wazi kuelezea yote waliyoyafanya katika majimbo yao na kuelezea maisha halisi ya familia zao ili jamii iweze kuwatambua zaidi.”
Pia jarida letu linawashukuru wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine wametuwezesha kufika miaka 11 ya usambazaji wa jarida letu la BANG! 
Kwa kuwezesha yote hayo jarida letu limeboresha zaidi kazi zake kwa kuzifanya ziwe na ubora unaokubalika kimataifa, hivyo ili kufanikisha hayo limepandisha gharama zake ili kuweza kufanikisha hayo yote.
Katika kusherehekea miaka 11 tunapenda kuwashukuru wadau wote wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadau wengine kwa ushirikiano wao wanaouonesha kwa jarida hili na kuliwezesha kufika mbali.
Lengo kubwa la jarida hili ni kuhakikisha kazi za wanawake wa kitanzania zinatambulika Afrika yote ili kuwawezesha kuinua uchumi wao kupitia kuibua vipaji vyao kwa kuziandika kazi zao ili waweze kutambulika
Asanteni kwa kunisikiliza.
Mkurugenzi wa BANG! Emelda Mwamanga.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...