Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Bi. Maryam Hamdani akifungua mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu Haki za binaadamu na sheria za waandishi wa Habari katika kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kiliopo Migombani.
Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mohd Khamis akiwasilisha mada ya Chimbuko, Historia na Maendeleo ya Haki za Binadamu Kimataifa, Kikanda na Tanzania katika mafunzo ya waandishi wa Habari yaliyofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Migombani.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo Salma Saidi akitoa muongozi kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Mwandishi Mkongwe wa habari Tanzania Salim Said Salim akiwasilisha mada ya Kanuni, Miiko na Maadili ya Waandishi wa Habari Kimataifa na kitaifa katika semina ya waandishi wa Habari iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji akiwasilisha mada juu ya Mapitio ya sheria za uandishi wa Habari Zanzibar.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo Bi. Maryam Hamdani (wa pili kulia) na washiriki wa mafunzo hayo.
Picha Na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment