Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akizungumza wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kujadili na kufanya uamuzi wa kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi katika wilaya ya Sumbawanga na Kalambo leo tarehe 23 Mei 2015. Kikao hicho kimeridhia mapendekezo hayo ya Halmashauuri husika baada ya kukidhi vigezo ambapo yatapelekwa ngazi za juu kwa uamiuzi zaidi.
Majimbo hayo yatazaliwa katika majimbo yaliyopo hivi sasa ambapo kwa jimbo la Kwela ambalo lipo katika Wilaya ya Sumbawanga litazaa jimbo la Ziwa Rukwa baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi ikiwemo ya idadi ya watu na ukubwa wa jografia. Kwa upande wa jimbo la Kalambo ambalo lipo katika Wilaya ya Kalambo linatarajiwa kuzaa Jimbo jingine la Mambwe. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa taarifa iliyopokelewa na ofisi yake kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya maelekezo ya kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni muwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama hicho Mkoa.
Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta.
Sehemu ya wajumbe na waalikwa wa kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment