Thursday, May 28, 2015

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YASAINI MKATABA WA KUBORESHA HUDUMA ZA UFUNDI WA VIFAA TIBA

af1
Dkt. Mmbando akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba huo  toka serikali ya korea ya kusini katika kutoa mafunzo kwa mafundi wa vifaa na vifaa tiba walioajiriwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya hapa nchini ili waweze kuongeza ujuzi katika matengenezo na kuboresha huduma ya ufundi.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowele
af2
Katibu mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na naibu meneja toka KOFIH wakisaini mkataba huo. Mkataba huo  utasaidia pia  kuboresha huduma za ufundi wa vifaa tiba katika karakana za ufundi wa vifaa tiba zilizopo katika hospitali za rufaa za kanda, rufaa za mikoa na hospitali za wilaya.
af3
Dkt. Mmbado akikabidhiwa mkataba huo toka kwa Naibu Meneja Gong, In Jae .
…………………………………………………………..
Dkt. Mmbando amesema ,  serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya imeendelea kuboresha upatikanaji na uwepo wa huduma ya vifaa tiba na mashine mbalimbali za teknolojia za kisasa katika ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za Afya kuanzia zahanati hadi hospitali ya Taifa. Ili kusimamia matumizi bora na kutunza raslimali hii kumehitajika kuweka juhudi za maksudi kuandaa wataalam wa ufundi wa vifaa tiba kwa kuwajengea uwezo katika kufahamu wa namna ya matengenezo ya mashine zilizopo na zinazo endelea kununuliwa; Pia kuwapa  vitendea kazi(tools kits, measuring and calibration equipment) vyenye kuwezesha mafundi kuhakiki ubora wa ufanyaji kazi kwa baadhi ya vifaa tiba mara baada ya kufanyiwa matengenezo.
“Kwa ushirikiano huu kati yetu na Korea ya Kusini ikiwa ni nchi iliyopiga hatua kubwa kiuchumi na teknolojia au miundombinu kwa ujumla wake ninaimani tutajifunza mambo mengi na kutoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya hapa nchini”.
Alisema kikubwa wamelenga kupata ujuzi zaidi kutoka kwao ingawa watagharimia masuala mengi katika mchakato mzima. Tunahitaji sisi wenyewe serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, Manispaa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za Afya vinapatikana na vinatumika kutoa huduma kwa wagonjwa muda wote vinapohitajika.|” Hili litawezekana kama tutatenga bajeti za matengenezo kinga(Planned Preventive maintenance) na kutumia wataalam wa ufundi wa vifaa tiba wanaotambulika “.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...