Friday, May 22, 2015

WAFANYABIASHARA WALEMAVU WAFUNGA BARABARA KWA SAA SITA KUPINGA KUBOMOLEWA VIBANDA VYAO NA MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM

 Wafanyabiashara walemavu wakiwa wamekaa katikati ya makutano ya barabara za Uhuru na Kawawa na kufunga barabara hiyo wakipinga kubomolewa vibanda vyao na Halmshauri ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam jana mchana. Halmshauri hiyo ilivunja vibanda hivyo kupisha upanuzi wa barabara.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio wakiwangalia wafanyabiashara hao walemavu walivyofunga barabara hizo.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wakifika eneo la tukio kupata suluhisho.
 Wafanyabiashara hao wakiwa wamekaa mbele ya malori wakizuia yasipite mpaka kieleweke.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiwaeleza wafanyabiashara hao maafikiano yaliyofikiwa na viongozi wao.
 Mmoja wa Wafanyabiashara hao akizungumza kwa hisia kali katika tukio hilo.
Baadhi ya utingo na vijana wakiwa wamekaa juu ya magari yao wakati wa sakata hilo. 
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)
……………………………………………………………………………………………
Na Chalila Kibuda,Globo ya Jamii
UMOJA wa Walemavu Wafanyabiashara  Mkoa wa Dar es Salaam (Uwawada),wamefunga barabara ya Uhuru na Kawawa kushinikiza serikali kutoa maelezo kuhusiana na  uvunjaji wa meza katika soko la Machinga Complex  unaodaiwa kufanywa na askari wa jiji, majira ya nne usiku wa juzi.
Wafanyabiashara hao wamekaa katikakati ya barabara kwenye makutano ya Barabara ya Uhuru na Kawawa  karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,ikiwa na lengo kutaka maelezo ya serikali kuu juu kufanya opresheni usiku bila kufanya ushirikishaji wa wahusika.
Akizungumza  na  waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,Kidumke Kidumuke amesema meza za walemavu zilizopo machinga Compelex ziliwekwa kutokana na makubaliano na kuamliwa kuweka meza hizo, lakini wamevunja utaratibu na kufanya  tuingia kufanya barabara bila utaratibu.
Kidumuke amesema kutokana uvunajaji huo walemavu baadhi wamepotelewa na mali zao na hakuna mtu ambaye atafidia hivyo kwa serikali inawajibika kulipa na makubaliano hayo yanatakiwa yawe katika maandishi.
Amesema walemavu tumekuwa tukionewa kutokana na hali zetu lakini leo tunawapa usumbufu wananchi ni kwa ajili ya kutaka haki zetu na tunawataka radhi watusamehe.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi amesema kuwa kuhusu fidia watafanya uchunguzi ili kuweza waliopotelewa na mali zao.
Mushi amesema walemavu watarudi katika maeneo hayo na waondoke eneo la barabara ili watu wengine waweze kufanikisha shughuli  zao .

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...