Thursday, May 28, 2015

HOSPITALI YA POLISI KILWA ROAD YAPATA VIFAA VYA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI


Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road. Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahmani Kaniki.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), akiongozana na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), kuelekea kwenye jengo litakalotumika kwa ajili ya kuhifadhia maiti  katika hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza  wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti vilivyotolewa na Serikali ya Misri kwa Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road Jijini Dar es Salaam.


 Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Kaniki akizungumza  wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, Richard Malika akitoa maelezo kuhusu mchoro wa jengo la kuhifadhia maiti linalojengwa  katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam wakimsikiliza.


SOURCE - Issa Michuzi

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...