Thursday, May 28, 2015

RAIS KIKWETE AWAAPISHA KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE NA BALOZI WA TANZANIA SAUDIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha  Balozi Liberata Mulamula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi Mulamula anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara hiyo na kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi  Mulamula  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha.
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mulamula Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Hassan Simba Yahya  kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo Balozi Yahya alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
 Mhe. Rais Kikwete akishuhudia Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Yahya  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha.
Mhe. Rais Kikwete akimpongeza Balozi Yahya mara baada ya kumwapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha, Mhe. Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi  wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mgaza alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu  na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
Rais  Kikwete akishuhudia Balozi  Mgaza  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha.
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mgaza Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza mara baada ya kuwaapisha katika nyadhifa zao mpya.
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja  na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa tatu kutoka kulia), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya,  Balozi Mgaza na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mabalozi wa Tanzania.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...