Meneja msaidizi wa uchangiaji wa hiari Matilda Nyallu wa mfuko wa pensheni wa (PSPF) akieleza namna ya mfuko wa Hiari unavyo kuwa na nijinsi gani utafaidika pindi unapo jiunga na kuwa mmoja wa wadau wa (PSPF)
Kushoto Muandaaji wa sherehe ya wanawake wajasiliamali Shamimu Mwasha ambaye ni mdau wa (PSPF) akitoa ufafanuzi wa sherehe hiyo na kuwakaribisha wageni walioweza kuhudhuriapembeni ni mshereheshaji wa sherehe hiyo Jokate Mwegelo.
Afisa wa mfuko wa pensheni wa (PSPF)kushoto Hadji Jamadary akiwa na balozi wa mfuko huo Flaviana Matata katika sherehe hiyo
Afisa wa mfuko wa pensheni David.M.Mgaka (kulia) akimuelekeza namna ya kujaza fomu ya kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari
Zuhra.H.Wendo ambaye ni Afisa katika mfuko wa pensheni wa (PSPF) kulia akiwa na mmoja ya wajasiriamali akimpa msaada wa kujaziwa fomu ya kujiunga na mpango wa (PSS).
Kushoto afisa wa (PSPF)Hadji Jamadary akimpa maelezo mmoja ya mjasiriamali aliye weza kutembelea meza ya PSPF
Maafisa wa mfuko wa Penheni (PSPF) wakiwa wanaelekezana kitu mara baada ya kufanya usajili wa watu kadhaa walio weza kujiunga na mfuko huo
Baadhi ya wanawake wajasiriamali wakiwa wameketi pamoja huku wakiendelea kupokea ujumbe mbalimbali kutoka kwa wanawake tofautitofauti waliokuwepo katika sherehe hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Wanawake wajasiriamali dar es salaam washerehekea pamoja katika hafra fupi iliyo andaliwa na mjasiriamali shamimu mwasha kwa lengo la kuendeleza kuwa na mahusiano mazuri katika shughuli zao za kuijenga nchi kwakutumia vipaji na ubunifu walionao ili kuhakikisha bidhaa mbalimbali zakitanzania hazikosekani katika soko la hapa nyumbani hata nje ya nchi
Mfuko wa jamii wa (PSPF) umeweza kuwaunga mkono wajasiriamali hao kwa kuwa miongoni mwa mfuko unaotoa huduma mbalimbali kupitia mafao yao kwakuwa kunamafao mbalimbali katika mfuko wa pesheni ambayo wao kama wajasiriamali wanaweza kuyamudu na hatimaye kufikia malengo waliyo jiwekea
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo Meneja msaidizi wa uchangiaji wa hiari Matilda Nyallu amesema mfuko wa jamii wa (pspf) ni mfuko unao jali kila mmoja na nimfuko ambao unakupatia wewe mtanzania faida maradufu kutokana na huduma zinazo tolewa kuwa za kiwango cha hali ya juu amesema kupitia mafao mbalimbali likiwemo fao la mikopo ya elimu,fao la ujasiriamali,nyumba na mengine mengi pia aliweza kuwaeleza kuhusu uchangiaji wa hiari ambapo kupitia uchangiaji huo mtu yeyyote anaweza akaumudu kutokana ni rahisi na inakiwango cha kawaida cha kuchangia .
“Napenda kuwaalika katika uchangiaji wa hiari utakao kuwezesha wewe mchangiaji kunufaika na mfuko wako kwa mambo mbalimbali huu ni mpango mpya ambao hauchagui kama unafanya kazi za kuajiriwa au zisizo za kuajiriwa pindi utakapo jiunga utaanza na kuchangia moja kwa moja ambapo kiwango cha chini cha kuchangia ni kiasi cha sh.10,000 kwa kila mwezi nawakaribisha wote (PSPF) ili muweze kupata huduma zilizo bora na zenye uhakika”
Mfuko wa pesheni wa (PSPF) ni kwaajiri ya wananchi wa Tanzania kutokana na huduma zinazotolewa kukidhi kiwango kwa watu wa aina zote hivyo kujiunga kwako na mfuko huu wa kijamii ni miongoni mwa mafanikio yako katika maisha yako kwani ndoto zako zitakuwa zinatimia kwa wakati
No comments:
Post a Comment