Thursday, May 28, 2015

TANZANIA KUTOA NAFASI ZAIDI KUWEZESHA WAKIMBIZI KUWA NA MAISHA YA KAWAIDA

DSC_0009Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa ndege Kigoma akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia) na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto) kwa ajili ya kutembelea na kuona changamoto katika maeneo maalum wanapohifadhiwa Wakimbizi. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma Abdulla Saadala.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
DSC_0014Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akisamiana na  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui (kulia) pamoja na viongozi wengine wa usalama wa mkoa wa Kigoma mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma akiwa na mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto).
DSC_0016Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiendelea kusamiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kigoma waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma.
DSC_0019Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui mara tu baada ya kuwasili akiwa amefuatana na Waziri Chikawe (hayupo pichani).
DSC_0018Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma mara tu baada ya kuwasili.
DSC_0024Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux (kulia) mara tu baada ya kuwasili mjini Kigoma tayari kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
DSC_0027Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akifafanua jambo kwa viongozi wenzake mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma. Wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux.
DSC_0036Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux kuelekea chumba maalum cha mapumziko mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma.
DSC_0049Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (katikati) walipokuwa kwenye chumba cha mapumziko.
DSC_0071Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kabla ya kusomewa kwa taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi mkoani Kigoma.
DSC_0099Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru akisoma taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Kigoma.
DSC_0113Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza kwenye mkutano wa kupokea taarifa fupi ya hali ya wakimbizi katika mji wa Kigoma na changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
DSC_0128Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia jitihada zilizofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi katika kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa haraka zaidi ili wakimbizi nao wafarijike kama binadamu wengine sambamba na sheria za Umoja wa Mataifa zinavyotaka. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na watatu kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
DSC_0134Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma.
DSC_0146Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akizungumza katika mkutano huo ambapo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa moyo wake wa upendo na kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi Wakimbizi kutoka nchi za jirani.
DSC_0163Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katika picha ya pamoja ya viongozi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa mkoa wa Kigoma sambamba wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopiga kambi mkoani Kigoma kuhudumia Wakimbizi.
…………………………………………………………………………….
Na Modewjiblog team, Kigoma
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Tanzania itatoa nafasi zaidi kuliko ya sasa ili kuweza kuwaweka wakimbizi wa Burundi wanaoingia nchini katika mazingira ya kuishi maisha ya kawaida.
Kauli hiyo ameitoa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma jana kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kujionea hali ilivyo akiambatana na watendaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini.
Alisema kama taifa wameona uwingi wa Wakimbizi na watatoa nafasi zaidi ili kuwezesha Wakimbizi hao kupata mahitaji yao ya msingi kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi.
Alisema katika kufanikisha suala la kuhudumia Wakimbizi wanaomiminika kwa sasa serikali itashirikiana na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha mahitaji ya msingi kwa Wakimnbizi hao yanapatikana.
“Wakimbizi wanahaki ya kulindwa na kuthaminiwa kama wananchi wa Tanzania, kwa hiyo serikali itatoa nafasi zaidi na tunashukuru msaada tunaopata kutoka kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kukabiliana na tatizo hili …,” alisema.
Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja wa Mataifa unatiwa shaka na hali ya kisiasa ilivyo nchini Burundi na kusema kuyumba kwa hali ya kisiasa kunaweza kuleta Wakimbizi wengi nchini.
Alisema kwa sasa Umoja wa Mataifa unafanya kazi na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na wanachama wengine wa jumuiya za kimataifa kuhakikisha kwamba hali ya usalama inarejea nchini Burundi.
Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatuliwa kwa mgogoro wa Burundi.
Rodriguez alisema Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa namna inavyoshughulikia Wakimbizi na kusema Umoja wa Mataifa unaangalia hali inayojitokeza Burundi kwa makini ili kusaidia Tanzania isilemewe na Wakimbizi.
Aidha alisema kwamba kitendo cha serikali ya Tanzania kutoa nafasi zaidi ya kuwezesha kusiwepo na msongamano wa Wakimbizi Nyarugusu kunaonesha ushirika wa kweli kati ya serikali ya Tanzania na jumuiya ya Kimataifa katika kushughulikia matatizo ya Wakimbizi.
Alisema hata hivyo kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya ni gharama kubwa na kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya.
Aidha alisema kwamba Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama shirika moja, chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) wameitikia wanavyostahili pamoja na changamoto nyingi walizokumbana nazo.
Changamnoto hizo ni pamoja na uwingi wa Wakimbizi waliokuwa wakimiminika, umbali uliopo wa kambi ya Kagunga ambako walikuwa wanafikia huku waliowengi wakiwa wanawake na watoto.
Alisema hata hivyo UNHCR walifanikiwa kuwasajili Wakimbizi hao na kuandaa mazingira ya ukazi wao katika kambi ya Nyarugusu. Aidha wamewezesha usafiri kwa Wakimbizi kutoka Kagunga hadi Kigoma.
Pia alisema IOM walifungua njia kutoka Kagunga hadi eneo jirani ambako Wakimbizi walipakia katika mabasi na kufika katika vituo walivyotakiwa kuwepo.
Pia UNICEF waliweza kusaidia maji na vifaa vya usafi kwa watoto na WFP wao walihakikisha chakula kinafikishwa hasa biskuti za kuongeza nguvu.
Aidha WHO wao walikuwa wanaisaidia serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Kipindupindu.
Aidha UNFPA walishughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Mratibu huyo alisema kwamba hata hivyo mambo yote hayo yasingefanikiwa kama si kwa msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Mratibu huyo alisema kuwa Mashriika ya Umoja wa Mataifa yameanza kupata fedha za kusaidia katika shughuli zao na kwamba kuna ahadi ya dola za Marekani milioni 12.
Alisema kwamba Umoja wa Mataifa umeona kwamba kutitirika kwa Wakimbizi hao kumeleta hali ngumu kwa serikali ya Tanzania na wakazi wa Kigoma.
Alisema wanatambua changamoto zinazoambatana na kuwa na kundi kubwa la Wakimbizi lakini wataendelea kuhitaji msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika kipindi hiki kigumu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...