Friday, May 08, 2015

UNESCO, SERIKALI WATIA SAINI MRADI WA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU

DSC_0023
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia), Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na mkalimani wa Balozi wa China wakifurahi jambo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani) akiwasili kwenye chumba cha mikutano Wizara ya Elimu kwa ajili ya hafla fupi ya kutiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini. (Picha zote na Zainul Mzige
DSC_0037
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimina kwa furaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na kushoto ni Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (aliyeipa mgongo kamera).
Na Modewji blog team
SERIKALI na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana wametiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini.
Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema mradi huo ni mkombozi mkubwa katika maandalizi ya kufundisha kwa kutumia Tehama nchini.
Alisema mpango huo wenye kuwezesha walimu kujifunza Tehama unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ambao ndio wamepitisha fedha zao UNESCO.

No comments:

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa  Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe ...