Friday, May 08, 2015

MKUTANO WA ISHIRINI WA WANAHISA WA BENKI YA CRDB WAFANYIKA ARUSHA

SAM_2438
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya Crdb  unatarajia kufanyika kesho  jijini Arusha.
SAM_2456
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei,kushoto ni Naibu Mkurugenzi mtendaji huduma mtambuka benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka,kulia ni Naibu Mkurugenzi mtendaji uendeshaji na Huduma kwa wateja CRDB Bw.Saugata Bandyopadhyay
SAM_2443
Baadhi ya sehemu ya waandishi wa habari kutoka jijini Arusha
SAM_2437
Godwin Semunyo Meneja mahusiano Benki ya CRDB
SAM_2432
Bi.Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na huduma kwa wateja akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB
SAM_2450
Kulia ni Katibu wa bodi ya CRDB John Baptist Rugambo,katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Frederick Nshekanabo,Kushoto Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na huduma kwa wateja
SAM_2454
Mwandishi kutoka TV1 Arusha Jane Edward akijaribu kuchukua taswira katika mkutano huo
SAM_2447
Kulia ni Ena Mwangama Meneja kitengo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu na Edwin Nchimbi Afisa masoko wakifatilia mkutano huo
SAM_2458
Kulia ni Meneja Usajili wa Hisa kuotaka Benki ya CRDB Emmanuel Ng'ui na Dorice Ngikari kutoka ofisi ya Katibu wakifatilia jambo
  SAM_2460
Mwandishi wa habari kutoka Mwananchi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Arusha Media Mussa Juma akiuliza swali kwa Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB Dr,Charles Kimei
******* 
Na Pamela Mollel-Arusha
Kufuatia anguko la shilingi ya Tanzania dhidi ya dola  wafanyabiashara nchini wametakiwa kuona kuwa ni fursa ya wao kijiinua kiuchumi katika biashara zao ndani  na nje ya nchi na kuachana na propaganda za wanasiasa ambapo wanalalamikia anguko hilo.
Ambapo hali hiyo imesababisha kupanda kwa bidhaa mbalimbali nchini hali inayotajwa kuongeza ugumu wa maisha ya wananchi sambamba na wafanyabiashara nchini ambao wananunua na kuagiza bizaa kutika nje ya nchi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei wakati akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya Crdb  unafanyika  jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha  Kimataifa AICC.
Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa Banki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo limekuwa ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ambapo faida  hiyo itawasaidia kuweza kupatia wanahisa hao gawio la shilingi 15 kwa kila hisa na idadi ya wanachama hao.
Ambapo mizania imeongezeka kwa asilimia 17 katika lengo lao katika mwaka huu ingawa soko limekuwa gumu kutokana na mfumuko wa bei uliopo sasa.
Dr,Kimei aliongeza kuwa kutakuwepo na ajenda mbalimbali katika mkutano huo mkuu ambapo moja ya ajenda ni kuangalia namna ya kukua zaidi na kuongeza mtaji wao na kuboresha mfumo mzima wa Tehama ili kuweza kukabiliana na wizi wa kupitia mtandao ili kuweza kuwahakikishia usalama wa pesa za wateja wao.
Aidha Banki hiyo inamkakati wa kuongeza mtaji wao ambapo wanatarajia kuongeza zaidi ya billion 100 ili kuongeza aman za banki na mtaji wao ili kuboresha huduma hizo  na kukuza rasilimali za banki hiyo.
Dr,Kimei aliongeza kuwa wanamkakati wa kupanua huduma zao katika nchi ya Burundi na nchi jirani ili kuweza kuwarahishishia wateja wao pindi wanapotoka na kutembelea nchi hiyo na kupata huduma ya miamala ya fedha.
Banki hiyo hivi sasa wanamawakala zaidi ya 575 ya fahari huduma na wanamashine ya zaidi ya 375 za kutolea pesa katika mikoa yote nchini ili kuwarahisishia wateja wao kupata huduma za kibenki.

No comments:

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa  Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe ...