Saturday, October 11, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA PPF MWANZA

D92A8892Jengo la Kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF lililozinduliwa rasmi na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mjini Mwanza jana jioni.
D92A9128Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni la PPF mjini Mwanza jana jioni.Wengine katika picha kutoka kushoto,ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana Wiliam Erio, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Adam Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF Bwana Ramadhani Kija, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo.
D92A9148Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio wakiangalia madhari nzuri ya jiji la Mwanza wakiwa katika jengo jipya la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF muda mfupi baada ya kulizindua mjini Mwanza jana jioni.
(picha na Freddy Maro)

No comments:

UJUMBE WA MAAFISA KUTOKA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA MISRI WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA TANZANIA

Leo, tarehe 23/04/2026 Makumbusho ya Taifa la Tanzania imepokea ugeni maalum kutoka Chuo cha Kijeshi Misri (Egypt War College) walioko katik...