Tuesday, October 07, 2014

NSSF FURSA SEMINA YAFANYIKA DODOMA

Msimu  wa Semina za Fursa zinazoendelea katika mikoa mbalimbali, licha ya kuwa ni Siku ya Sikukuu ya Idd El Hajj, Fursa Semina ilishamiri mjini Dodoma na kuvutia umati mkubwa wa watu.
Umati huo ulivutiwa na huduma na mafao yatolewayo na NSSF kama vile Matibabu Bure kwa mwanachama na wategemezi wake, mikopo kupitia Saccos, Mafao ya kuumia kazini, Pensheni ya Uzeeni, Pensheni ya Urithi, Msaada wa Mazishi na Pensheni ya Ulemavu.
NSSF iliwasihi watu wajiunge na mfuko huo ili waweze jipatia Fursa za kuboresha maisha yao ya sasa na ya baadae.

Semina ya Fursa Dodoma ilirushwa Live na kituo cha Redio cha Clouds FM katika mkoa wa Dodoma  na hivyo kuwapa Fursa hata wale walioshindwa kufika ukumbini kufuatilia mada mbalimbali zilizotolewa popote walipo ndani ya mkoa huo.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa kwanza kulia), Meneja wa NSSF
Mkoa wa Dodoma,  Kirondera Nyabuyenze (wa pili kulia) na Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba  (wa tatu kulia) wakiwa katika semina ya Fursa
Dodoma.
 Mkuu wa Idara ya
Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume (wa tatu kushoto) na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Kirondera Nyabuyenze (wa pili kushoto) wakifutilia kwa
makini mada iliyokuwa ikitolewa katika semina ya Fursa Dodoma.
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa mada katika Semina ya Fursa
Dodoma.
 
 Baadhi ya watu
waliohudhulia semina hiyo 
wakiskiliza
kwa makini Fursa zitolewazo na NSSF.

Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa watu waliohudhuria semina hiyo.
 Mwanamuziki wa kizazi
kipya Mwasiti Almasi akiwahamasisha wananchi waliohudhuria semina hiyo
wajiunge na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili waweze jipatia Fursa
za kuboresha maisha yao ya sasa na ya baadae. Kushoto ni 
Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba 
 Maofisa wa NSSF, Gabriel Nkakatisi (kushoto) na Anna Nguzo
wakiandikisha wanachama wapya baada ya kumalizika kwa semina ya Fursa
iliyofanyika siku ya sikukuu ya Idd El Hajj mjini Dodoma.
Baadhi ya watu wakijiandikisha
katika banda la NSSF baada ya semina ya Fursa
Dodoma. 

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA PANGANI, AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI TANGA

PANGANI, TANGA – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 26, 2025, amezungumza na wananc...