Friday, October 31, 2014

BREAKING NYUZZZ......... :BASI LA SIMBA MTOTO LAGONGANA USO KWA USO LA LORI KWENYE DARAJA LA WAMI LEO


Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga likiwa limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani,dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.

CCM YAPOKEA KWA FURAHA FRELIMO KUIBUKA ,MSHINDI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MSUMBIJI

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,makao makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.
 ………………………………………………………
NA BASHIR NKOROMO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa furaha Chama cha Frelimo kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu.
Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Frelimo, Filipe Nyusi ameibuka kidedea na sasa ndiye Rais Mteule wa Msumbiji ambaye baada ya kuapishwa atashika mikoba itaakayoachwa na Rais anayemaliza muda wake, Armando Gwebuza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (Pichani), amesema, CCM imepokea ushindi huo kwa furaha kubwa kutokana na undugu wa damu uliopo baina yake na Frelimo kwa mikaka mingi.
“Chama Cha Mapinduzi kilifuatilia kwa karibu kwa kuwa CCM na Chama cha Frelimo ni vyama ndugu vyenye historia moja na ya pamoja ya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Historia hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Mteule wa nchi hiyo Ndugu Filipe Nyusi mara baada ya kuteuliwa kwake na Frelimo kugombea Urais, nchi ya kwanza kuitembelea kuwa Tanzania”, alisema Nape na kuongeza;
“Ikumbukwe kwamba huyu si mgeni hapa Tanzania. Kama wanaharakati wengine wa ukombozi, Ndugu Nyusi aliishi Tanzania, anaongea vizuri Kiswahili na anaichukulia Tanzania ni nyumbani”.
Alisema kwa mnasaba huo, Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa ujumla wana kila sababu ya kushangilia ushindi walioupata ndugu zao wa Frelimo, kwa kuwa ushindi huo ni wa wote.
“Tunampongeza sana Rais Mteule Filipe Nyusi kwa kupeperusha vema bendera ya Frelimo. Matokeo ya Uchaguzi yamedhihirisha imani kubwa waliyonayo wana-Msumbiji kwa Frelimo na kwa Rais Mteule Filipe Nyusi”, alisema Nape.
Nape amesema CCM ina imani kwamba chini ya uongozi imara wa Mwenyekiti wake Dk. Jakaya Kikwete, na Rais Mteule Filipe Nyusi, uhusiano kati ya vyama vya CCM na Frelimo utaimarika na kustawi.
Kadhalika Chama Cha Mapinduzi kimempongeza  Armando Guebuza kwa kuiongoza Frelimo na Taifa lake vema na kukamilisha uongozi wake kwa mafanikio makubwa.
“Anapoanza kipindi hiki cha uongozi wa Taifa lake, sisi wana-CCM tunamtakia Ndugu Nyusi afya njema, busara, maarifa na uongozi uliotukuka”, alisema Nape.
Alisema, CCM itasimama pamoja na Frelimo katika kuendeleza urithi ulioachwa na waasisi wa vyama vyao, Mwalimu Julius Nyerere na  Samora Machel.

SKYLIGHT BAND INAKUKARIBISHA USIKU WA LEO THAI VILLAGE KWA BURUDANI YA KIPEKEE KABISA!

DSC_0159Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba pamoja na Sam Mapenzi.
DSC_0007Aneth Kushaba sambamba na Digna Mbepera wakiwapa raha mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye show zao za kila Ijumaa ndani ya ukumbi wa maraha wa Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0012Kifaa kipya cha Skylight Band Bela Kombo akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi wa Thai Village Ijumaa iliyopita.
DSC_0024Kutoka kushoto Bela Kombo, Hashim Donode na Digna Mbepera wakiporomosha burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai Village.
DSC_0057Binti mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Digna Mbepera kwenye hisia kali za muziki wa Live kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0026Burudani ikiendelea.
DSC_0109

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YAMALIZA ZIARAYAKE KATIKA MGODI WA BUZWAGI

unnamedNaibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Wa kwanza kulia ni Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
unnamed1Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiambatana wajumbe wa Kamati katika ziara ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji katika mgodi wa Buzwagi.
unnamed2Pichani ni ujenzi wa awamu ya pili wa Kituo cha Afya cha Mwendakulima kinachojengwa na Mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kuwasogezea wananchi huduma bora za afya.
unnamed3Baadhi nyumba zitakazotumiwa na waganga na wauguzi wa kituo cha afya cha Mwendakulima pindi kituo hicho kitakapoanza kutumika.

TABATA FC YAINGIA ROBO FAINALI YA LIGI YA DK. MWAKA SPORTS EXTRA NDONDO CUP BAADA YA KUIFUNGA SIFA POLITAN KWA PENALTI 4-3


 Wachezaji wa timu za Boom FC na Vijana ya Ilala wakisalimiana kabla ya mchezo wao wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
 Kikosi cha timu ya Vijana ya Ilala kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Boom FC katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha timu ya Boom FC kikiwa katika picha ya pamoja.
 Mashabiki wa timu ya Boom FC, wakipiga ngoma wakati timu yao ikicheza na Vijana ya Ilala.
Nahodha wa timu ya Vijana Ilala (kushoto) akisalimiana na mwenzake wa Boom FC, kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.
Mshambuliaji wa timu ya Vijana Ilala, Matola Selemani, kushoto akiwania mpira na winga wa timu ya Boom FC, Nambongo Hussein katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.
Mshambuliaji wa timu ya Boom FC,Issac Tesha (katikati) akijaribu kufunga  bao katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 
Winga wa timu ya Boom FC, akiwatoka mabeki wa timu ya Vijana ya Ilala katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup. 
Beki wa timu ya Vijana Ilala Ramadhani Yasini, (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa timu ya Boom Ally Kondo, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.     
Baadhi ya wadau wa  Soka wakifuatilia mechi kati ya Tabata FC na Sifa Politan kwenye Uwanja wa Bandari.  
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Sifa Politan, Mathayo Edward (kulia) akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa timu ya Tabata FC, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Bandari Dar es Salaam. Tabata ilishinda kwa Penati 4-3.    
 Mashabiki wa timu ya  Sifa Politan wakishangilia timu yao.
 Mashabiki wa timu ya Tabata FC wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Sifa Politan kwa mikwaju ya penalti 4-3.
 Kipa wa Sifa Politan akiruka bila mafanikio kujaribu kuokoa penalti iliyopigwa na Kudura Shaban wa Tabata FC. 
Heka Heka katika lango la timu ya BOOM FC.
 Mashabiki  soka wakifuatilia pambano la Sifa Politan na Tabata FC kwenye Uwanja wa Bandari.
Wadau wa Soka wakifuatilia pambano la Sifa Politan na Tabata FC kwenye Uwanja wa Bandari.
 Mashabiki  soka wakifuatilia pambano la Sifa Politan na Tabata FC kwenye Uwanja wa Bandari.
 Mashabiki wa timu ya Tabata FC wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Sifa Politan kwa mikwaju ya penalti 4-3.
Mashabiki wa timu ya Tabata FC wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Sifa Politan kwa mikwaju ya penalti 4-3.
SOURCE: issamchuzi.blogspot.com

Thursday, October 30, 2014

BUNGE LA BURKINA FASO LACHOMWA MOTO

Waandamanaji wakilitazama bunge la Burkina Faso likiteketea kwa moto.
Waandamanaji hao wakishangilia baada ya kuchoma bunge.…
Waandamanaji wakilitazama bunge la Burkina Faso likiteketea kwa moto.
Waandamanaji hao wakishangilia baada ya kuchoma bunge.
Magari nayo yameteketezwa kwa moto.
WAANDAMANAJI nchini Burkina Faso leo wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga kupitishwa kwa katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongeza muda wa kukaa madarakani.
Rais Compaore anataka kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia kuliongoza taifa hilo.
Taarifa kutoka Mji Kuu ya nchi hiyo, Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama tawala na makao makuu ya chama hicho cha Congress for Democracy and Progress yamechomwa moto pia.
Bunge hilo lilitaka kubadili katiba itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia madarakani tangu mwaka 1987 ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani.
Kumekuwepo kampeni za wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Kabla ya kuchomwa moto bunge hilo, polisi walilipua mabomu ya machozi kuwazuia waandamanaji waliokuwa wakielekea katika jengo la bunge hilo japo takribani watu 1,500 walifanikiwa kupenya na kulichoma bunge hilo.
Waandamanaji walionekana wakichoma nyaraka na kupora baadhi ya vifaa vya kompyuta huku magari yaliyokuwa nje ya jengo hilo nayo yakichomwa moto.

TIM COOK WA KAMPUNI YA APPLE ASEMA ANA FAHARI KUWA SHOGA

Mtendaji Mkuu wa Apple, Tim Cook.
MTENDAJI Mkuu wa kampuni ya Apple ya Marekani, Tim Cook, amefichua kwamba yeye ni shoga na anaona fahari kuwa hivyo.
Cook ameyasema hayo leo katika tahariri ya mtandao wa Businessweek.com kwamba: “Acha niseme wazi. Ninaona fahari kuwa shoga, na ninaona kuwa shoga ni moja ya zawadi kubwa zaidi ambazo Mungu amenipa.”
Ameongeza kusema kwamba wafanyakazi “wengi” wa Apple wanafahamu kwamba yeye ni shoga na haoni tofauti yoyote kuhusu wanavyoshirikiana naye.
Cook anakiri kwamba jambo la kufichua hali hiyo halikuwa rahisi, lakini alifanya hivyo kwa kutaka jamii imwone yuko sawa na watu wengine.
“Sijioni kuwa mwanaharakati katika jambo hili, bali ninatambua nilivyonufaika katika kujitoa mhanga kwa wengine.
Hivyo, iwapo kusikia kwamba mkuu wa Apple ni shoga kunaweza kumsaidia mtu fulani kuelewana na wengine, au kumfariji mtu yeyote anayejihisi kuwa mpweke, au kumtia moyo mtu apiganie usawa katika jamii, basi kujitoa kwangu mhanga kujifichua katika hali hii ni jambo zuri,” alisema.
Kampuni ya Apple kwa muda mrefu imepigania usawa kwa wafanyakazi wake kwa kushirikiana na Tim Cook.
Kampuni hiyo pia ilipinga wazi muswada wa bunge la Jimbo la Arizona ambao ungewaruhusu wafanyabiashara kuwabagua watu kwa misingi ya dini.
“Kampuni ambayo nina bahati kuiongoza imekuwa ikipigania haki za binadamu na usawa siku zote,” alisema Cook na kuongeza: “Tutaendelea kupigania haki zetu, na ninaamini mkuu yeyote wa kampuni hii kubwa, bila kujali rangi za watu, jinsia, au mwelekeo wa kujamiiana, atafuata msimamo huu.
Na mimi nitaendelea kupigania usawa wa watu wote hadi kieleweke.”

SERIKALI YAAHIDI KUTAFUTA UFUMBUZI SUALA UHABA WA MAGHALA

…………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Waziri Mkuu Mizengo  Pinda amesema  Serikali imeanza kulifanyia kazi tatizo la wakulima kukosa mahali pa kuhifadhia ya mazao yao, hivyo  litapatiwa  ufumbuzi katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo baada ya mpango wa kujenga maghala makubwa kuanza.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda  katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Julius  K.Nyerere  uliopo jijini Dares Salaam kufuatia ya ziara yake ya kikazi katika nchi za Uingereza, Poland na Oman. yenye lengo la kuhimarisha mahusiano.
Waziri Mkuu Pinda alisema ametembelea nchi ya Poland, ambayo ilikuwa na lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano na kutafuta msaada wa mfumo wa mkopo wenye masharti nafuu wa kusaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala  kwa ajili ya kuhifadhia nafaka au chakula.
Alisema katika nchi hiyo amejionea jinsi ilivyo kuwa na mfumo  maalum  wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chakula.
“Unahitajika mfumo huu wa Poland wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi  chakula. Hivyo tunahitaji kiasi cha fedha cha  Sh.  bilioni 240 hadi  bilioni 260  kwa ajili ya kukabilian na tatizo hili, tumeandika ombi na tumeshapeleka  kwa Serikali,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
 Aliongeza kwamba  pia wameomba mkopo wenye masharti nafuu ili kusaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia chakula, hivyo kwa kuanzia wameomba mkopo wa Euro milioni 500 katika nchi ya Poland,ambao wenye riba  nafuu ya kiasi cha 0.25.
 Alisema lengo ni kujenga maghala kubwa katika  baadhi ya mikoa, ambayo aliitaja kuwa ni  Rukwa, Ruvuma, Iringa, Njombe, Dodoma,  Tanga na ghala dogo katika  Kanda ya Ziwa.
Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mahindi nchini alisema wakulima wameweza kuzalisha tani 500,000 za mahindi, lakini changamoto iliyopo iliyopo   ni mahali pa kuhifadhia.
 Aliongeza kuwa uwezo wa maghala ya  Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula(NFRA) ni tani 240,000  wakati bado kuna tani zaidi ya 200,000 zilizozalishwa mwaka jana (msimu uliopita) za mahindi na katika kipindi cha sasa wamepanga kununua  tani 3.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali imeshirkisha sekta  binafsi ili iweze kununua tani 200,000 na lakini bado chakula ni kipo cha kutosha.
 Alisema kwa upande wa mpunga kuna tani zaida 800,000 kwani msimu huu zilimezalishwa tani milioni 1.5. hali hiyo imechangiwa na matumizi ya mbegu bora, mbolea na  matumizi ya matrekta.
Waziri Mkuu aliwapongeza wakulima kwa juhudi zao za kulizalisha chukula cha kutosha.
Akizungumzia kuhusu ziara yake nchini Oman alisema ilikuwa na lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.
Alisema nchi hiyo mwikitio wa nchi hiyo wa kuwekeza ni mzuri hususan kwenye kilimo, mifugo na uvuvi.
“ Eneo walioonesha hisia ni la mifugo,  hasa

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...